Mafunzo ya watu wazima leo 23

LESONI, FEBRUARI 23

SOMO: “MASIHI” WA KIUAJEMI (ISA. 44:26—45:6)



Ni utabiri upi wa kushangaza hutokea katika Isaya 44:26—45:6?



Huduma ya Isaya ilidumu kuanzia mwaka 745 K.K. hadi kufikia 685 K.K. Baada ya mshindi atokaye mashariki na kaskazini (Isa. 41:2, 3, 25), na kumaanisha kwamba hii ingelikuwa habari njema kwa Yerusalemu (Isa. 41:27), Isaya kwa usahihi alimtabiri Koreshi kwa jina na kuelezea kazi zake. Alitokea kaskazini na mashariki ya Babeli na kuishinda katika mwaka wa 539 K.K.; alimtumikia Mungu kwa kuwaachilia huru Wayahudi kutoka katika uhamisho wao wa Babeli; na alitoa amri ya kuijenga upya hekalu la Yerusalemu (tazama Ezra 1). 



Weka utabiri huu katika mtazamo mpana. Kwa kuwa kuna takriban miaka mia arobaini na sita tangu kipindi cha kufa kwa Isaya hadi anguko la Babeli, unabii wake ulikuwa karne moja na nusu baada ya wakati wake. Ingekuwa kama vile George Washington akitabiri kwamba mtu aliyeitwa Generali Dwight Eisenhower angeisaidia kuikomboa Ulaya katika mwaka 1945! 



Kwa sababu vitendo vya Koreshi vinashuhudiwa katika vyanzo mbalimbali vya kale, ikiwemo vitabu vya mambo ya nyakati za Babeli, taarifa yake mwenyewe “Silinda ya Koreshi,” na Biblia (2 Nyakati. 36:22, 23; Ezra 1; Dan. 5; Dan. 6:28; Dan. 10:1), usahihi wa unabii wa Isaya hauwezi kupingwa. Hii huthibitisha imani ya watu waaminio kwamba manabii wa kweli hupokea tabiri za kweli kutoka kwa Mungu, ajuaye mambo ya siku za usoni muda mrefu kabla ya kutimia. 



Kwa nini Mungu humwita Koreshi “mtiwa mafuta Wake” (Isa. 45:1)?

Neno la Kiebrania linalomaanisha “mtiwa mafuta” hapa ni neno ambalo kutokana nalo tunapata neno Masihi. Kwingineko katika Agano la Kale, hili neno lingetumika kwa kuhani mkuu mtiwa mafuta (Walawi. 4:3, 5, 16; Walawi. 6:22), mfalme wa Israeli mtiwa mafuta (1 Sam. 16:6; 1 Sam. 24:6, 10; 2 Sam. 22:51), au Masihi, mfalme kamili ajaye kutoka katika ukoo wa Daudi na Mkombozi (Zab. 2:2; Dan. 9:25, 26). Kwa mtazamo wa Isaya, Koreshi alikuwa mfalme ajaye, aliyetumwa na Mungu kuwakomboa watu Wake. Lakini hakuwa masihi wa kawaida, kwa sababu hakuwa Mwisraeli. Angefanya mambo fulani ambayo Masihi angeyafanya, kama vile kuwashinda maadui wa Mungu na kuwaacha huru watu Wake walio utumwani, lakini asingekuwa kama Masihi, kwa sababu hakutokea katika uzao wa Daudi. 



Kwa kumtabiri Koreshi, Mungu aliuthibitisha Uungu wake wa kipekee kwa kudhihirisha kwamba ni Yeye pekee aujuaye wakati ujao (Isa. 41:4, 21—23, 26—28; Isa. 44:26). Pia alimwahidi Koreshi: “Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa Mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli (Isa. 45:3). 



Fikiria kuhusu unabii mwingine uliotimia kama ulivyotabiriwa (kama vile falme za Danieli 2 isipokuwa wa mwisho, Danieli 7, au kuhusiana na wakati wa Kristo katika Danieli 9:24—27). Ni tumaini gani unabii huu hutupatia kama watu binafsi? 

No comments