ndoa yangu

NDOA YANGU

Sehemu ya ( 01)

Niliwahi kuambiwa kwamba katika maisha kuna mtihani ambao unazawadiwa cheti halafu kisha mtihani unafuata,na mtihani wenyewe huo si mwingine bali ni ndoa,siku ya kuzawadiwa cheti huwa ni siku ya furaha na yenye kuhudhuliwa na watu wengi,lakini baada ya hapo watu hao hao waliokuwepo wanakuzawadia cheti sasa inakuwa ni zamu yao kukutazama unavyopata taabu katika mitihani

Leo mimi Janeth najikuta nimekaa peke yangu nalia,machozi ninayolia si ya furaha kuonyesha nimefaulu mtihani,hapana bali ni ya uchungu na fedheha kuonyesha ile mitihani niliyokabidhiwa imenishinda.

Nailaani nafsi yangu na elimu yangu kukutana na Maiko katika masomo yangu,mwanaume ambae leo amenifanya nimeinamia goti langu saa hizi huku nikilia kwa uchungu.

Naomba sasa nikuhadithie ili kama unachakunishauri nijifunze
......Mapenzi Mapenzi Mapenzi,kwa kweli ni bora uyasikie tu yakisemwa lakini moyo wako usije ukadhubutu kumpenda mtu mpaka ukajihisi kichaa,Nakumbuka kipindi nikiwa kidato cha pili nilikutana mvulana mmoja anaekwenda kwa jina la Maiko,Mvulana ambae niliingia nae kwenye uhusiano nikiwa katika ngazi hiyo ya elimu,umri wangu ulikuwa mkubwa kwa sababu sisi zamani unakuta mtu unaanza kidato cha kwanza ukiwa mtu mzima kabisa,hii ilitokana na kucheleweshwa kuanzishwa shule,ila leo siwashauri kabisa endapo kama kuna watoto wanasoma hii simulizi mje mfanye michezo ya mapenzi mkiwa mashuleni.

Nikili wazi tu kwamba Maiko aliuteka moyo wangu kwa asilimia mia moja,alinifanyia mengi mazuri ambayo yalisababisha nizidi kuweka jeraha la upendo wa dhati ndani ya moyo wangu juu yake,Zaidi alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana darasani,alinisaidia mengi sana hasa katika swala la elimu,nakumbuka sikumoja wakati ananifundisha somo la fizikia aliniambia"Namuandaa mke wangu wa baadae ili pindi mimi nikiwa daktari basi yeye awe daktari wangu msaidizi,".Maneno haya nayakumbuka vizuri sana na kwa msaada wake mpaka ninavyozungumza hivi mimi ni muuguzi wa hospitali moja hapa dar es salaam.

Upendo ulikuwa mkubwa sana na hakika tulifanyiana mengi yasiosahaurika yaliyosababisha kutengeneza cheni yenye mnyororo mzito wa upendo.
Tulishakamatwa sana na waalimu na tukaonywa sana,wakati mwingine tulipewa adhabu lakini ndani ya adhabu ile kwetu sisi tuliona kama furaha ya kutufanya tuzidi kuwa pamoja,Nakumbuka siku moja mwalimu wa  zamu alitupa adhabu ya kuchimba shimo,lakini adhabu ile tuliifanya kwa pamoja,badala ya kuichukia adhabu tulijikuta tukifanya kazi kwa mshikamano huku tukiwa na furaha kuwa pamoja.Hakika haya ndio yalikuwa maisha yetu.

Penzi na masomo viliendelea na hatimae kidato cha nne kiliwadia,Maiko alikuwa mstari wa mbele kwa kunihimiza nisome kila,aliniletea maswali na kunisaidia kuyafanya,pia aliniletea vitabu mbalimbali ambavyo nilijikuta na mimi navisoma kwa bidii,Maiko alichangia sana mimi kuipenda shule,bado naendelea kuikumbuka kauli yake kila mara,Alisema"nafanya hivi kwa sababu nakuandaa wewe mke wangu wa baadae ili uje unizalie watoto wazuri na wenye akili wawe wasomi kama wewe mke wangu",Ki ukweli kauli zake zilinifanya nijiskie raha kila mara na zaidi zilinogesha upendo,kutokana na upendo huo nilijikuta wanaume wengine wote nawaona kama tu kaka zangu wa kuzaliwa nao tumbo moja hivyo sikuhitaji kusikia habari za maswala ya mahusiano kutoka kwao.

Siku zilisogea na hatimae mtihani tulifanya,Kwa kweli namshukuru sana Maiko kwani baada ya kumaliza mitihani kwa asilimia mia moja ufaulu ulikuwa ni wangu,Siku hazigandi tarehe ya matokeo kutoka ilifika,Shule yetu ilijitahidi sana kwa kufaurisha wanafunzi,moja kati ya waliofaulu vizuri jina langu lilikuwemo japo maiko aliongoza kwa shule nzima,Hakika hayo ndio yalikuwa maisha yetu,nashukuru sana kwa sababu alikuwa mstari wa mbele kuniandaa kama mke wa baadae,hakutaka tu kunitumia na kuniacha bali alinisihi sana katika upande wa masomo pia na mimi kujikuta napenda masomo yangu.

Hatimae safari ya kidato cha tano ilianza,katika uchanguzi wa shule tuliambizana tuweke shule yenye mchanganyiko wa wavulana na waschana ili ikitokea tumechaguliwa pale basi tuwepo wote pamoja.Ni kama wapangaji walikuwa upande wetu kwani tulijikuta tuko pamoja tena katika elimu ya kidato cha tano na cha sita,huko tulikuwa kama vile mapacha,mara nyingi wakati wa kusoma tulisoma pamoja,tulikula pamoja ki ukweli kwa kila shughuri ambazo zilitukutanisha wasichana na wavulana tulifanya pamoja,hakuacha kunisaidia katika masomo yangu maana wote tulikuwa tukisoma masomo yale yale ya sayansi.
Tulipanga mambo mengi ya maisha ya baadae na hata juu ya watoto wetu pindi tulipokuwa tukipata muda wa mapunziko,hakika yalikuwa ni mahusiano ya kupendeza japo tulijua tukifanya makosa kujihusisha na mapenzi shuleni

Hakuna kipindi muda unapokuwa mdogo kama kipindi cha mtu kuwa na furaha,nilifurahia sana maisha yale ya kidato cha tano na cha sita lakini yalikuwa mafupi sana kwangu,Tulijikuta tunafanya mitihani na kurudi nyumbani tukisubiri matokeo tena,kila mmoja aliludi kwa wazazi wake,richa ya kurudi nyumbani bado hakukunizuia mimi kukosa muda wa kuiba iba kuonana na maiko.tuliishi maisha hayo na sasa hatimae kwa mara nyingine matokeo ya kuelekea elimu ya juu yalitangazwa,nashukuru Mungu tulifaulu japo Maiko alinizidi tena.Hii haikuwa na shida ila shida ilianzia hapa:.

Siku moja Maiko alikuja kwangu akiwa mnyonge,siku hiyo sintaisahau katika maisha yangu kwani ni siku ambayo nililia sana,Maiko aliniambia kwamba Baba yake amepata uhamisho kutokana na ile kazi anayofanya kwenye kampuni yake ya biashara,Kiongozi mkuu wa kampuni amemuhamisha na kumpa makazi uingereza kwa ajiri ya kwenda kukaa kule ili awe anasimamia soko la ukusanyaji wa bidhaa kule ili awe anazituma huku wa ajili ya kuuzwa.
Kwa kweli baada ya kusikia hili swala pumzi ilinishuka,akaendelea kusema kwamba...Wataondoka yeye na familia yote ndani ya kesho kutwa na masomo yake yote yatakuwa kule,
Ki ukweli kwa kauli hii nilijikuta nalia kama mtoto kwa kumkosa maiko karibu yangu mtu ambae alikuwa nguvu ya kusonga mbele katika mafanikio yangu.

Nakumbuka ndio ilikuwa siku ya mwisho kuonana na Maiko niliongea mengi sana siku hiyo ambayo mengine mpaka nimeyasahau,Maiko nilimshuhudia akitoa machozi ya uchungu kwa kunikosa tena karibu yake,kulikuwa hakuna namna na wala hatukuweza kupinga amri ya baba yake.

Kweli siku ya kesho yake sikuweza kuonana nae kabisa kutokana na yeye kuwa bize na upangaji wa vitu kwa sababu ya safari,siku iliofuata nilimshuhudia maiko wangu ndani ya kioo cha gari akinipungia mkono wa mwisho huku akiwa anaelekea airport kwa ajili ya kupanda ndege.

Maisha ya upweke yalianza,kila mara nilimkubuka Maiko wangu,Muda wa kuanza chuo ulifika,niliomba kusoma kozi ya uuguzi,kila mara nilipokuwa chuo nilijihisi mpweke,nilimkosa maiko tena katika mawasiliano kama unavyojua zamani teknologia ilikuwa bado haijakua,mwaka wa kwanza ulipita ndani ya upweke.

Miaka haichelewi na hatimae upweke kwangu ulinishinda,na hapo ndipo nilipokutana na kijana Greyson,kijana ambae ki ukweli sikumpenda kama maiko lakini basi tu niliingia nae kwenye mahusiano kwa sababu nilichoka kuwa mpweke,Uhusiano mimi na Gryson uliendelea mpaka siku namaliza chuo kikuu,Mahusiano yetu yaliendelea japo tulimaliza chuo pamoja baada ya miaka mitatu ya kukaa chuo,Nilikaa mwaka mmoja nyumbani lakini maisha yangu yote nilikuwa nikimkumbuka Maiko,sikuwahi tena kuwasiliana nae na sasa miaka minne imepita na sasa nikapata kazi,niliona Maisha ya Maiko yalishakuwa ya huko na sijui sasa hivi anafanya nini huko.Mara ikafika wakati sasa Grey anataka kunioa sikuwa na jinsi maana umri ulikuwa umeenda na sasa nilihitaji kuwa na mwenza wangu.Ama hakika ndoa ilifungwa na maisha ndani ya pete yalianza,siku zote hizo sikumsahau Maiko ndani ya moyo wangu alikuwa ni mwanaume pekee sana niliempenda.

Miaka mitatu ilipita ya ndoa na sasa nilikuwa na mtoto mwenye miaka takribani miwili,Siku yenyewe ilikuwa siku ya mapunziko nikiwa nyumbani jikoni na mume wangu akiwa sebureni nilishangaa kuona namba ngeni ikiita kwenye simu yangu,nilijua labda ni watu wa kikazi hivyo niliipokea.Sikuamini masikio yangu kwa kile nilichokisikia kwani nilisikia sauti ikisema"Hallow mpenzi wangu wa dhati Janeth ni mimi Maiko,Za Miaka??"...Kujibu nilishindwa na hata kuongea nilishindwa,aliendelea kuongea na kusema "nipo dar es salaam saa hizi nimetelemka na ndege toka jana uko wapi Janeth wangu".Kwa uchungu nilijikuta nikilia huku nikikosa cha kufanya,Nilikata simu ili nielekee chumbani niweze kulia vizuri,Kilichoniliza na kuniuliza maswali je ikiwa Maiko amekuja kwa ajili ya kunioa nitafanya nini mie na wakati ndie mwanaume pekee nimpendae kwenye hii Dunia..?Niliiangalia namba yake mara mbilimbili na kujiuliza endapo nikimpigia simu nianzie wapi pa kuongelea japo najua aliempa namba huenda tayari kamuelezea yote juu yangu.

JE NINI KITAENDELEA

Tukutane sehemu ya pili.

Mwalimu Habel Noah

No comments