ndoa yangu
NDOA YANGU
Sehemu ya (02)
Ilipoishia
... Niliiangalia namba yake mara mbilimbili na kujiuliza endapo nikimpigia simu nianzie wapi pa kuongelea japo najua aliempa namba huenda tayari kamuelezea yote juu yangu.
Sasa endelea
Kabla hata sijachukua maamuzi yoyote simu ilianza tena kuita,kuangalia ilikuwa namba yake,sikutaka kupokea maana nilikuwa bado nalia,sasa nikaanza kufuta machozi ili nijitengeneze vizuri kisha nipokee,nilifanya hivyo wakati huo na yeye hakuchoka kupiga simu japo ilikuwa haipokelewi.
Sasa nikawa nimejiweka sana na hatimae nae akapiga na mimi nikapokea"Hallow"....Niliitikia kinyonge sana kama vile mtu mgonjwa."Hallow Janeth wangu kwanini ulikata simu yangu na ukawa hupokei tena.....usiwe na hofu nimeshaambiwa kila kitu kwamba umeolewa na unamtoto mmoja".
Niliposikia kasema hivyo moyo ulipiga paaaah!! na mara nikaanza kusikia maumivu ya uchungu,aliendelea akasema"Ni kweli tumeachana kwa mda wa miaka mingi lakini kule uingereza nilikuwa nasomea masomo ya udaktari ambayo yamenichukua mda mrefu sana kuyamaliza,nashukuru Mungu nilimaliza salama na nikapata ajira huko huko hivi hapa nipo likizo nikasema ngoja nije Nyumbani huku Tanzania".Aliongea maneno yale yaliyozidi kuniumiza na kunifanya nijiskie uchungu zaidi,"Janeth naomba tuonane japo nikuone nimekukumbuka sana,usiwe na shaka mimi najua kila kitu hivyo ntaonana na wewe tu kama rafiki kwa sasa kwa sababu najua kwa sasa una mme wako."Nilijikuta nashindwa la kuongea zaidi ya kuitikia tu kipole"Sawa".
Tulikaa tukapanga tuonane kesho yake eneo flani mida ya jioni,na hakika nilikuwa na hamu sana ya kumuona Maiko mwanaume niliempenda kwa dhati,Ki ukweli niliona kesho yake inachelewa,nilijaribishia kila nguo ambayo ningeona ingenipendeza kwa siku ya kesho,Muda wote nikawa na tabasamu japo uchungu moyoni wa kumkosa Maiko katika ndoa ulikuwepo,mara kwa mara nilikuwa nikiumia kwa kuyakumbuka maneno yake kwamba anataka tuzae watoto wenye akili ambao watakuwa wasomi kama mimi,nilikuwa nikifikilia hilo naumia sana kushangaa watoto hao nimekuja kuzaa na mwanamme ambae sikuwa nampenda kutoka ndani ya moyo.
Hatimae kesho yake jioni ilifika,tulipeana ahadi tukutane katika hotel moja hivi na kweli Maiko alikuwa mtu wa kwanza kufika,Sikuamini macho yangu kukutana na Maiko kwa jinsi alivyobadilika,alikuwa na umbo zuri la ki utu uzima na mwonekano mzuri kuliko hata kipindi tunasoma,moyo ulizidi kuniuma zaidi hasa kila nilipokuwa nikimwangalia.
Siku hiyo tulikaa,tukala na kunywa pia tuliongea mengi sana na kukumbushiana mengi mno ya kipindi cha shule,nilijikuta ni mtu mwenye furaha kama vile ni mume wangu kabisa,nilijikuta nacheka kwa kujiachia utafikiri tupo Dunia ya peke etu.
Hatimae muda ukawa umeenda ilibidi tuagane na kupeana ahadi tusiache kuwa tunaonana mara kwa mara.Niliondoka na kurudi nyumbani,Mume wangu Grey sikumkuta bali nilimkuta tu msaidizi wetu na mwanangu,nilishukuru Mungu maana nilikuwa nimekwepa maswali ya ulikuwa wapi.
Hatimae kadri siku zilivyozidi kwenda tulijikuta mazoea ya ukaribu zaidi yanarudi,kama waswahili wasemavyo penzi la kweli halifi ndivyo ilivyotokea kwetu kwani licha ya mda mchache kuwa karibu tulijikuta tena tumerudi katika maswala ya mahusiano.Nilijikuta siku nyingine nikitoka kazini nabadilisha nguo na kuondoka kwenda kuonana nae,mara nyingi nilimdanganya sana mme wangu kuwa ni mambo ya kazi kumbe ilikuwa uongo mtupu.
Sintasahau katika maisha yangu siku moja tukiwa katika chumba cha wageni mimi na Maiko ilikuwa ni siku ya mapumziko,mlango uligongwa na tulipouliza ilisikika sauti ya muhudumu,nilinyanyuka nikiwa nimejifunga taulo za mle chumbani kwa ajiri ya kwenda kumsikiliza,sikuamini macho yangu na nilihisi kuzimia baada ya kukutana na sura ya mume wangu Greyson akiwa na rafiki zake watatu,nilianza kurudi kinyume nyume na hatimae aliingia ndani na kukutana na Maiko.
Mme wangu hakusema maneno mengi bali alianza kwanza kulia kiume kwa kuonyesha machozi yakimdondoka shavuni"nimeanza kukufuatilia toka zamani sana,toka ulipoanza kubadilika na sasa nimejua sababu ni nini kumbe hii ndio tabia yako na hichi ndicho kilichokufanya uwe na dharau na kunidhalilisha kiasi hiki....Janeth hebu niambie nimekukosea nini katika maisha yangu au nimekunyima nini katika maisha yangu mpaka ufikie kitendo cha kunifanyia haya,nashukuru sana ukitoka hapa njoo nyumbani chukua kilicho chako uende kwa huyu bwana wako mimi na wewe basi umenitukana vya kutosha".
Grey alitoa bahasha ya kaki na kuichana,picha nyingi za ki mahaba zilizoonyesha kila nilipokuwa nikitoka naenda kukutana na Maiko zilionekana,kumbe alianza uchunguzi zamani sana ndio maana nilikuwa nashangaa kila nikitoka nikirudi na yeye simkuti nyumbani kumbe alikuwa akinichunguza."mchezo wako nimeujua toka zamani sana sasa na leo ndio mwisho wa mimi na wewe kwaheri ya kuonana".Grey alianza kuondoka huku akitokwa na machozi nilipiga magoti na kumshika miguu kumuomba msamaha lakini haikuwezekana.Waliondoka pasipo kumfanya chochote kile Maiko zaidi waliishia tu kumuangalia
Maiko alibaki akiangalia tu yaliyokuwa yakiendelea huku moyo wake ukiwa na wasi wasi juu ya ujio ule,nilimwangalia na kujikuta nimepata hasira na kujutia niliyoyafanya,Maskini Grey wangu aliondoka, nilivaa haraka na kuanza kumfuata nyumbani baada ya mimi pia kuchukua usafiri.Nimkuta ameshafika nyumbani zamani sana na tayari ameshafungasha kila kilicho changu na kukiweka mlangoni.
Hakuniruhusu hata kuingia ndani zaidi alizungumza kitu kimoja tu"unajua kwanini sikumfanya chochote huyo bwana wako??....nimeishi nikikupeleleza siku zote kupitia mazungumzo yako ya simu na hata pindi mlipokuwa mkikutana nimekuja kugundua kwamba ni mtu unaempenda na mlietoka nae mbali na siwezi kuvuja upendo kwa kusema nikupige wewe au nimpige yule ndio maana nilimwacha....Mungu awajaalie maisha marefu kwaheri Janeth".Grey aliyasema hayo na kufunga mlango,nilijitahidi sana kulia na kugonga mlango lakini hakuna alienisikiliza,nilipiga kelele za kuomba msamaha lakini hazikuzaa,mwisho wa siku nililudi mlangoni na kuanza kulia mwenyewe na kujutia yale niliyoyafanya,nilijisemea moyoni"Maiko hawezi kunioa tena,tayari nina ndoa na mtoto na hata hivyo hapa yupo likizo tu ya muda mfupi,nitaishi maisha gani mie"Taratibu usingizi ulinipitia nikiwa pale mlangoni.Maana tayari usiku ulikuwa umeshaingia sana.
JE NINI KITAENDELEA
Usikose sehemu ya tatu.
Post a Comment