CEDRIC KAZE AUKUBARI MZIKI WA SIMBA

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa Simba ina wachezaji wazuri na wenyeji uzoefu wa kutosha kama wataamua kupambana watafika mbali kwenye mashindano ya Kimataifa (Caf Champions League).

Kaze amewapa nafasi Simba ya kufuzu robo fainali kama wachezaji wataamua kujituma na kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo kwenye mechi za makundi. Pia amewaomba mashabiki wa Simba na watanzania kwa ujumla kuisapoti Simba katika hatua hiyo.

Moja ya faida kubwa ya timu kufika hatua za makundi , robo fainali , nusu fainali au fainali... ni kutambulisha ubora wa ligi ya nchi husika . Hivyo tuwe sawa kuwaombea wenzetu hao kufanya vyema katika safari yao pia na wale wengine Namungo.
#BinagoUPDATES

No comments