amka na Bwana leo 19
KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA, FEBRUARI, 19, 2021
SOMO: AMANI KATIKA UWEPO WAKE
Nitayakumbuka matendo ya BWANA, Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.
Zaburi 77:11, 12.
Mambo makubwa yako mbele yetu, na tunataka kuwaita watu kutoka katika kutofautiana kwao, kujiweka tayari kwa ajili ya siku ile .... Hatupaswi sasa kuutupa ujasiri wetu, bali kuwa na uthibitisho imara, imara zaidi kuliko hapo kabla. Hata sasa Bwana ametusaidia, na atatusaidia hadi mwisho. Tutatazama katika minara ya kumbukumbu, ukumbusho wa kile Bwana alichotutendea, kutupatia faraja na kutuokoa toka katika mikono ya mharabu.
Tunataka kuwa na kumbukumbu kwa upya ya kila chozi ambalo Bwana amefuta toka katika macho yetu, kila maumivu aliyotuliza, kila hofu aliyoondoa, kila wasiwasi aliofukuza, kila hitaji alilotupatia, kila rehema aliyotupatia, na kututia nguvu kwa ajili ya yote yaliyo mbele yetu kupitia ukumbusho wa kusafiri kwetu. Tunaweza tu kutazama mbele katika pambano linalokuja, lakini tunaweza kuangalia katika kilichopita pia na kile kitakachokuja, na kusema, “Hata Sasa BWANA ametusaidia” (1 Samweli 7:12). “Na Kadiri ya siku zako, ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako” (Kumbukumbu La Torati 33:25). Jaribu halitazidi nguvu tutakayopewa ili kuistahimili.
Hivyo tuendelee na kazi kuanzia pale tunapoikuta, pasipo neno moja la kulalamika, kwa kufikiria kuwa iwepo chochote kitatukabili ile nguvu itakuja kulingana na jaribu. Watoto wetu wapo mikononi mwa Mungu. Imani yetu sharti iamke ili kushikilia ahadi na tusilalamike, tusihuzunike, kwani kwa kufanya hivyo hatumheshimu Mungu. Tunapaswa kutumainisha msimamo wa moyo mchangamfu na wenye matumaini. Amani yetu ya sasa isisumbuliwe na majaribu yajayo, kwa kuwa Mungu hataiacha wala kuikataa roho moja inayomtumainia.
Mungu ni bora sana kwetu kuliko hofu zetu. Ikiwa tungeendeleza kwa bidii ukumbusho na masimulizi ya rehema zetu, tukihesabu mifano ambayo Bwana ametenda kwa ajili yetu, imekuwa bora kwetu kuliko hofu zetu, mifano ya alivyoingilia kati kwa uweza na neema yake tulipofadhaishwa peke yetu, kututegemeza wakati wa kuanguka, kutufariji wakati wa kuhuzunika, tungeona ya kwamba ni kukosa imani kutokumtumainia Mungu au kujawa na hofu. Rehema na zikumbukwe na kufurahiwa kila siku. Tunapaswa kuishi kwa imani kila siku.... Furahini katika Mungu kila mara zote. Leo msifu Mungu kwa neema yake, na endelea kumsifu kila siku.
Post a Comment