mafunzo ya watu wazima leo 19
LESONI, FEBRUARI 19
JIFUNZE ZAIDI:
Soma Ellen G. white, "Mtazame Mungu Wako!" katika Prophets and Kings, uk. 311—321.
“Katika siku za Isaya uelewa wa kiroho wa wanadamu ulitiwa giza kutokana na kutokumtambua Mungu. Kwa muda mrefu Shetani alitafuta kuwasababisha wanadamu kumtazama Muumbaji wao kama mwanzilishi wa dhambi, mateso na kifo. Wale aliowadanganya hivyo, walidhani kwamba Mungu alikuwa mkali na dhalimu. Walimtazama kama anayetazama ili kushutumu na kuhukumu, asiye tayari kumpokea mwenye dhambi kwa kadri kulivyokuwa na udhuru wa kisheria wa kutomsaidia. Sheria ya upendo inayoongoza mbingu haikueleweka kwa mdanganyifu mkuu akiuchukulia kama mipaka katika furaha ya wanadamu, nira ngumu ambayo wanapaswa kufurahi kwa kuiponyoka. Alitangaza kwamba sheria zake zisingeweza kutiiwa na kwamba adhabu za makosa hazikutolewa kwa usawa.” —Ellen G. White, Prophets and Kings, uk. 311.
MASWALI YA KUJADILI:
1. Fupisha kwa maneno yako mwenyewe ujumbe wa Isaya 40:12—31. Iandike kwa kutumia picha za kisasa, kama vile ugunduzi wa sayansi ya kisasa unaoonesha kwa dhahiri zaidi uweza wa Mungu wa kutisha. Elezea kwa ufupi katika darasa lako.
2. Nikwa namna gani maelezo ya Isaya kuhusu kudumu milele kwa Neno la Mungu dhidi ya ufupi wa maisha yenye kuharibika ya mwanadamu (Isa. 40:6—8) hukupa ufahamu kuhusiana na hofu yako ya kifo? Ni kwa vipi yanahusiana na tumaini lako la ufufuo (Ayubu 19:25—27, 12 Dan. 12:2, 1 Kor. 15:51—57, 1 Thesal. 4:13—18)?
3. Kwa kutafakari moyoni Isaya 40:12—31, mtu anawezaje kuponywa kutokana na kiburi na majivuno?
Muhtasari: Kupitia kwa Isaya, Mungu alileta faraja kwa wale waliokuwa wanateseka. Muda wao wa mateso ulifikia ukomo, Naye Mungu alikuwa anawarudia. Kuliko kukatishwa tamaa na kuchanganyikiwa, wangemtumaini Mungu kutumia uweza wake wa uumbaji kwa niaba yao.
⏰
Post a Comment