YANGA YAINGIA KAMBINI LEO HII

YANGA YAINGIA KAMBINI LEO
 
Baada ya kupewa mapumziko ya siku 10, kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo kuanza maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom itakayorejea Februari 13 pamoja na michuano ya kombe la FA.

Wachezaji wa kigeni waliotumia mapumziko hayo kusafiri makwao kuziona familia, walianza kuwasili jana huku wengine wakitarajiwa kutua leo.

Nahodha Lamine Moro, mlinda lango Farouk Shikhalo ni miongoni mwa nyota wa kigeni ambao walirejea siku ya jana.
#BinagoUPDATES

No comments