WAZIRI DOROTHY GWAJIMA ASEMA BIMA YA AFYA RUKSA KWA WOTE
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hoja ya uwasilishaji wa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote katika Bunge la Mwezi September mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu (Afya), Edward Mbanga ametooa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambapo taasisi zilizo chini ya Wizara ziliwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu yao.
Mbanga amesema mapitio ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 yanaendelea, kwa kuifanyia maboresho zaidi ya kisera ikiwemo sehemu ya makundi yaliyopaswa kupewa msamaha wa matibabu kwa kutokua na uwezo wakiwemo wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi, watoto chini ya miaka mitano, akina mama wajawazito na wagonjwa wenye maradhi ya muda mrefu.
#BinagoUPDATES
Post a Comment