unabii sehemu ya 8,kunene kinyume aliyejuu(Mungu)

PEMBE NDOGO ILINENA MANENO KINYUME CHAKE ALIYE JUU.(Aliye Juu ni MUNGU)

UNABII:sehemu ya nane.

Maranatha!

Naamini ndugu msomaji hujambo katika BWANA 🙏🏻. Nakukaribisha tena katika somo tajwa hapo juu. Tutajibu hoja kwa kutumia biblia, Roho ya Unabii na rejea kutoka kwa waandishi wa kanisa katoliki.

Kama tulivyokwisha jifunza huko nyuma kuhusu huyu pembe ndogo kuwa ni ufalme wa kidini ambao unawakilishwa na kanisa la roman Catholic . Pope wa Vatican ni kiongozi wa kiroho na kisiasa katika kanisa hilo. Wapo mapapa wengi sana ambao wamepita katika kanisa hilo, mapapa huchaguliwa na kuwekwa katika cheo hicho na baada ya hapo yeye Pope atadumu kuwa kiongozi mkuu katika kanisa hilo hadi mwisho wa maisha yake, yani kifo ndo kitamtoa hapo, labda itokee tu dharula. Huo ni Uongozi wa kifalme wa dunia hii katika hilo kanisa, ndio maana tunasema pembe ndogo ni ufalme wa kidini/serikali ya kidini.

2Wathesalonike 2:4
👉🏻Yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu , ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la MUNGU akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye MUNGU .

Danieli 7:25
👉🏻Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu.

Aliye Juu ni MUNGU pekee.

Kunena maneno kinyume cha MUNGU ni KUKUFURU.  Je ni mamlaka gani iliyofanya hivyo???

Katika ombi kuu la YESU la Yohana 17:11 YESU anasema "NAMI NAJA KWAKO BABA MTAKATIFU"

Na katika Mathayo 23:9 YESU anatuambia sisi Wanadamu hivi "WALA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI , MAANA BABA YENU NI MMOJA ALIYE MBINGUNI"

Ni MUNGU Pekee ndiye BABA MTAKATIFU.  Lakini kuna mtu duniani naye anaitwa baba mtakatifu, papa anajiita baba mtakatifu, je siyo kufuru hiyo???

Marko 2:7
YESU alipomwambia yule mgonjwa, mwanangu umesamehewa dhambi zako, wayahudi walimwambia YESU kuwa anakufuru, maana anayesamehe dhambi ni mmoja tu naye ni MUNGU BABA MTAKATIFU ALIYE JUU MBINGUNI .

Lakini kanisa katoliki limejichukulia mamlaka ya kusamehe dhambi. Pope anayejifananisha na MUNGU yeye pia husamehe watu wake dhambi. Je hii siyo kufuru??

JE NDANI YA KANISA LA ROMANI CATHOLIC PAPA AMEJIKWEZA HATA KUJIFANANISHA NA MUNGU??

Hebu vitabu vyao viseme vyenyewe👇🏻👇🏻👇🏻

LUCIUS FERRARIS , PROMPTA
BIBLIOTHECA , POPA ART. 2

👉🏻PAPA anauwezo mwingi na nguvu, kwamba anaweza kurekebisha na kuelezea au kufafanua hata amri takatifu.

👉🏻Papa anaweza kurekebisha Amri takatifu, kwa maana nguvu siyo za mwanadamu bali zile za MUNGU , na hutumika kama makamu wa MUNGU duniani.

LUCIUS FERRARIS, PROMPTA BIBLIOTHECA
      VOL 6, p 29

👉🏻Lakini sasa papa anajiita Vicar of son of God(aliye badala ya mwana wa Mungu)

👉🏻Papa anaheshima ya hali ya juu kiasi kwamba yeye si mwanadamu wa kawaida , lakini kana kwamba ni makamu wa MUNGU .

👉🏻Papa kwa utukufu hujiona hana kasoro kuitwa bishop wa Mabishop. Yeye pia (papa) ni kiongozi wa KRISTO (Yesu) na mfalme wa Mfalme(Yesu).

👉🏻Basi ndiyo maana anayo taji ya ngazi tatu, kama mfalme wa mbinguni na duniani na hata chini ya dunia.

Hivi ni vitabu vyao wenyewe ndo vinafafanua jinsi Pope wa Roma alivyojaa majina ya makufuru. Majina ya MUNGU na sifa za MUNGU Aliye Juu, hii ndume imejichukulia tu kinguvunguvu.

Mungu ashukuriwe kwa kuwa hawa watu hawadumu milele, maana kama wangeishi milele bila kufa, dunia yote ingeliamini kuwa papa ni MUNGU . Ni MUNGU pekee asiyepatikana na mauti. Yeye anaishi milele. 

Rafiki wasomaji, MUNGU awasaidie mpate kuijuwa iliyo kweli kupitia neno lake ili mpate kuokolewa.

BWANA awabariki mnapotafakari neno hili zuri linalotolewa bure, ili tupate wokovu.

BWANA awakumbuke! Katika Jina la Yesu!

               Amina!🙏🏻

No comments