JPM; WALIOKIMBIA HOSPITALI ZA SERIKALI WALIPE GHARAMA WALIZOSOMESHEWA
Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa wizara ya afya kuwafuatilia watumishi wote waliokimbia vituo vya afya vya serikali baada ya kupangiwa warejeshe gharama walizosomeshewa na serikali. Rais ameyasema hayo akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora baada ya kupata taarifa kwamba watumishi kadhaa wamekimbia katika hospitali hiyo na kwenda kuajiriwa katika hospitali za watu binafsi.
Kwa kawaida mkataba ambao madaktari na watumishi wengine wa afya ambao huwa wanaosomeshwa na wizara ya afya degree ya pili huwa kuna kifungu kinachomtaka mtumishi huyo baada ya masomo kufanya kazi na serikali kwa muda wa miaka mitatu vinginevyo analazimika kurudisha gharama.
#BinagoUPDATES
Post a Comment