unabii sehemu ya 6,Pembe ndogo yafanya vita na watakatifu

PEMBE NDOGO ILIFANYA VITA NA WATAKATIFU.

UNABII:sehemu ya sita.

Danieli 7:21
👉🏻nikatazama na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu ikawashinda.

Nawasalimu wote katika jina la YESU 😅 aliye Hai! Ni matumaini yangu kwamba mu wazima na mnaendelea vema na majukumu yenu😅. Wapendwa ndugu zangu nawakaribisheni tena katika muendelezo wa somo tajwa hapo juu👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Somo lililopita la sehemu ya Tano tuliona kwamba anayewakilishwa na pembe ndogo ni UFALME WA KIDINI YANI KANISA LA ROMAN CATHOLIC AMBALO KIONGOZI WAKE MKUU DUNIANI NI PAPA ALIYE NA MAMLAKA YA KIROHO NA YA KISIASA. Hii mamlaka ni ya kidini lakini kuna jambo tena inalifanya ambalo ni ajabu kwa Taasisi ya kidini kulifanya🤔

Danieli alionyeshwa kuwa mamlaka hii itafanya vita na watakatifu tena itawashinda.

Kanisa la Rumi ya Kikristo liliposhika hatamu ya Uongozi duniani, lilitunga mafundisho yake lenyewe ambayo lilitaka kila mtu ayakubali, wao kama wakatoliki hawaamini Biblia ila huamini mapokeo yao. Ili kanisa hili liweze kuwadhibiti wote ambao watapingana na mafundisho yao na kumpinga papa wa roma, lilianzisha mabaraza ya kuwanyamazisha wote ambao watasimamia ukweli ulioandikwa katika BIBLIA ,  hivyo mahakama za kukomesha uasi zilianzishwa na Taasisi hii ya kidini ili kuzima kile walichokiita uzushi juu ya kanisa la Roma .

Utawala huu wa pembe ndogo ulienea kote, uliwashawishi wafalme wa dunia hii kumkiri na kumtambuwa papa kuwa ni wakili wa MUNGU duniani. Wafalme wengi walijiweka chini ya utawala huu na kupokea maagizo kutoka ikulu ya papa. Wakristo wanamatengenezo katika nchi za ulaya ndiyo walikuwa wahanga wakubwa wa mateso makali. Watu wengi waliompinga papa waliuawa kikatili kwasababu ya kusimamia haki na neno la MUNGU . Wengi walihukumiwa na mahakama za hili kanisa la Roma . Akina martin Luther, akina john huss, akina Wycliffe na wafuasi wao wengi mno walikinywea kikombe kichungu cha mateso kutoka Roma ya kidini. Kule ufaransa mauaji ya kutisha yalienea nchi nzima, Wakristo wa kweli walikamatwa na kuchinjwa hadharani wakiitwa wahaini na wazushi dhidi ya kanisa. Wakati mmoja waprotestanti kule ufaransa walikuwa wamelala , maelfu ya waprotestanti walikusanywa usiku huo na kupelekwa kuuawa, mauaji hayo ya watu waaminifu kwa MUNGU yalidumu kwa siku saba katika mji wa parisi, kwa amri ya mfalme aliyekuwa akipokea maagizo kutoka rumi, mauaji yaliendelea hadi kufika katika miji mingine. Kwa kifupi ufaransa ilichafuka kwa damu, kule poland pia mauaji ya watakatifu wa MUNGU yalifanyika, pande zote utisho wa pembe ndogo ulienea. Simba walikula nyama za watu katika viwanja vya michezo, wateule walipelekwa katika viwanja vilivyojaa watu watazamaji ili kuona jinsi wanavyopoteza maisha kwa njia ya uchungu.
Habari za mauaji kila zilipofika ikulu ya Roma, viongozi walifurahi.

Katika kipindi hicho cha utawala wa pembe ndogo, watu milioni hamsini walilala mauti.

Kipindi upapa ulivyokuwa na mamlaka kuu ulaya, wanahistoria hutuambia kuwa mamilioni ya watu waliuawa kwasababu walikataa kuyatambuwa mamlaka ya papa kama kanisa la kweli duniani.

Papa Martin wa tano aliyetawala mwaka 1417 hadi 1431, alimwambia mfalme wa poland kuhusu WAKRISTO wafuasi wa John Huss, wajibika kuwaua wafuasi wa John Huss.

Mpendwa msomaji, Bila shaka leo unaona dunia imetulia, kila mahali, kila nchi inahubiri amani! Amani! Amani! Umoja umoja umoja, je unadhani kutakuwa na amani na umoja?? MUNGU anasema hakutakuwa na amani na wala hawatashikamana. MUNGU ameshatuambia, kwamba yale yaliyotendeka huko nyuma dhidi ya watu wake waaminifu katika zama za giza yatajirudia tena na mda si mrefu. Waweza jisemea kuwa hilo haliwezekani kutokea, watu wameelimika, dunia ina wasomi wenye busara, kuna watetezi wa haki za binadamu, katiba zetu zinaruhusu uhuru wa dini na kuabudu, nakuhakikishia ndugu msomaji kuwa hayo yote ni bure, lazima unabii utimie ili YESU arudi. Yote yatatimia hakika.

Leo tunashuhudia upapa ukiita jamii ya Wanadamu wote duniani kuungana na kuwa wamoja, wamoja katika imani bila kubaguana, kufundisha kitu kimoja katika imani zote, tunaishi tukishuhudia muungano wa dini duniani kote, muungano wa dini tayari umeshaanzisha mabaraza yao, yote haya yanatimia machoni petu lakini watu hawaamki.

Ajenda za mabadiliko ya tabia nchi zinasukumwa na Pope wa Vatican katika mataifa yote duniani, nyuma yake kuna siri iliyofichika na wengi hawajui, ila watakuja kujuwa wakiwa tayari wamefungwa matitamatita tayari kwa kuchomwa moto.

Ujumbe wa malaika watatu uliokabidhiwa kwa Waadventista wasabato kama ungehubiriwa kwa nguvu, bila woga, na watu wote wangekuwa wameonywa, tungeshuhudia hasira ya Joka. Ajabu ni kuwa Waadventista Wasabato wameuacha ujumbe huu na sasa wamejiungamanisha na jumbe laini laini zisizogusa mioyo ya dhambi, jumbe ambazo BWANA hajawatuma, wachungaji wanasafiri safari ndefu lakini hawana ujumbe, wainjilisti wanasafiri safari ndefu lakini pia hawana ujumbe wa malaika watatu. Fedha ya MUNGU inatumika tu kufurahisha watu badala ya kuwaonya, hii fedha kila aliyesafiri na hakutoa ujumbe wa onyo kwa watu, MUNGU atamuwajibisha, lazima mzitolee hesabu siku yaja.

Wasabato wa leo uoga umeingia ndani ya mioyo yetu. Waoga, na wasioamini , MUNGU amesema hawataingia MBINGUNI bali sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto. Ufunuo 21:8

Niwaulize Waadventista WASABATO wenzangu, hivi mnadhani  kwenda MBINGUNI njia  ni tambarare??? Hakika njia imesonga sana, ina vitisho tele, lakini BWANA MUNGU anataka tupite njia hiyo. Ukristo siyo lelemama, Ukristo ni gharama, utatugharimu uhai, mali na yote tuliyonayo.

YESU anataka tuhubiri ujumbe wa wakati huu na siyo kuhubiri hadithi hadithi mimbarani wakati roho zinazingirwa na ibilisi, waambieni watu kweli yote bila kuwaficha. Hali ya hewa inaelekea kubadilika, mda siyo mrefu mataifa yatazibadili katiba za nchi zao na kuingiza sheria ya utunzaji wa siku ya kwanza ya juma jumapili kwa lazima.

Mpendwa msomaji, nimalizie kwa kusema hivi, Chini ya uongozi wa rumi ya kidini, wale walioteseka kwaajili ya injili walishutumiwa kama watenda maovu, wakihesabiwa katika jamaa ya Shetani . Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwetu sasa. Shetani atawaletea mateso wale wanaoishika sheria ya MUNGU ili washitakiwe kuwa ndio wanaosababisha maafa duniani . Atajitahidi kuwatisha kwa njia ya hofu, akiwachochea watu pamoja na serikali wapingane na sheria ya MUNGU .

Wale wote wanaoiheshimu sabato ya biblia watashutumiwa kuwa ni maadui wa nchi, wavunja sheria ya jamii, watu wakorofi wasio na utaratibu, na ndio wanaosababisha maafa haya yote. Wasabato waaminifu watashitakiwa kila pembe ya dunia kuwa ni wahaini walio kinyume na sheria za nchi.

Ujumbe wetu kwa Wanadamu wa leo ni ujumbe wa kufa na kupona. Ukipewa nafasi kuhubiri kumbuka ujumbe wa malaika watatu, usiogope! Malaika wako karibu yako hata kama waumini na viongozi watakutenga, mbingu hazitakutenga, wewe ni mwana wa Mfalme wa wafalme .

Endelea kufatilia somo la 7 katika mfululizo huu wa ujumbe wetu. Waambieni Waadventista kwamba wasiogope hasira za Joka,  YESU alishamponda shetani kichwa, Yeye Kristo atatupigania na kamwe hatotusahau.

BWANA awabariki .🙏🏻

Share ujumbe huu kwa wengine wengi hapa chini kupitia mitandao ⏬ 

2 comments:

  1. Mungu mkuu tusaidie!mafunzo haya ni mazuri,subir ni share kwa wengine zaidi,barikiwa mtumishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen,🙌🙏barikiwa zaidi,na share kwa wapendwa tujifunze sote!😇

      Delete