CLORIS LEACHMAN
Mwigizaji mkongwe wa filamu za vichekesho wa nchini Marekani, Cloris Leachman amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 94.
Bi. Leachman alifariki usiku wa Jan. 26 2021 nyumbani kwake huko Encinitas, California akiwa na binti yake, Dinah Englund.
Leachman ni kati ya waigizaji wanaoheshimika na waliofanikiwa kwa ukubwa hata kuteuliwa na kushinda tuzo kubwa na maarufu Duniani za Emmy na Oscar.
Leachman enzi za uhai wake ameigiza kwenye filamu maarufu kama vile ‘The Women’, ‘The Beverly Hillbillies’, ‘S.O.S. Titanic’, miongoni mwa nyingine nyingi.
R.I.P Cloris Leachman.
#BinagoUPDATES
Post a Comment