machapisho ya kishetani

_MACHAPISHO YA KISHETANI NDANI YA NYUMBA ZA UCHAPAJI ZA SDA.

MANUSCRIPT RELEASE . 1273 - Machapisho ya Kishetani katika Nyumba za Uchapishaji za Kanisa la Waadventista Wasabato; Yoshua, Kuhani Mkuu, Ashtakiwa*_

_*"Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake." [ Ufunuo 14: 6-8 ]. 17MR 236.1*_

_*"Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata," Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili una umuhimu mkubwa, na unafuatwa na ujumbe wa malaika wa tatu. Zote tatu zinapaswa kueleweka na kuwekwa pamoja. Onyo lililomo katika ujumbe huu lina maana kubwa kwa ulimwengu wote zaidi ya watu wengi wa Mungu wanavyofahamu. Tuko katika siku kuu ya Bwana ya matayarisho. 17MR 236.2*_

_*Shetani anaangalia vituo vyote kuona ni wapi anaweza kuuingia  mlango wa kuingilia. Kwa miaka amekuwa akitenda kwa udanganyifu wake wote wa udhalimu kupata nafasi ya kusimama katika nyumba ya uchapishaji ya Review na Herald. Na ameipata. Ameruhusiwa kuja mahali ambapo inapaswa kuchukuliwa kuwa takatifu, mahali patakatifu, hekalu la Mungu, ambalo Bwana angepeleka miale ya mwangaza iliyo wazi, angavu kwa sehemu zote za ulimwengu. Shetani amefanikiwa kuweka mikononi mwa wafanyakazi wa nyumba zetu za uchapishaji kundi la wataalamu wa sanaa ya uandishi ambalo limeandaliwa kudanganya, ikiwezekana, wateule. Jambo lenye makosa hatari limeletwa katika ofisi yetu ya uchapishaji, na makosa haya yameendelezwa kwa kuchapishwa kwenye matbaa zetu na kuchapishwa katika mfumo wa kitabu. Kanuni hizi za uovu zimeathiri akili za wale ambao wameshughulikia jambo hili. Matokeo yake, roho zitapotea kwenye kusudi la Mungu. Tayari wengine wamekaribia kupoteza akili zao za utambuzi kati ya ukweli na uongo. 17MR 236.3*_

_*Hata watu ambao wanajitahidi kuinua mawazo yao wenyewe kama ujuzi wa kushangaza wanastaajabu kwamba watu walio katika nafasi za uwajibikaji katika idara yetu ya uchapishaji-idara ya uchapishaji iliyowekwa kulinda ukweli wa Mungu-wamekubali kuchapisha vitabu vyao. Ili kufanya kazi hii ya nje, mameneja wa nyumba ya uchapishaji wamepuuza kufanya kazi ambayo walipaswa kufanya. Kazi ya kidhehebu (Kanisa la Mungu) imecheleweshwa, wakati kazi ya kibiashara, ambayo inapaswa kufanywa kuwa ya pili kwa umuhimu kwa jukumu letu wenyewe, imefanywa kuwa ya kwanza. Wafanyakazi wameshughulika na vitabu vyenye nadharia zenye kudhoofisha kiroho. Wametumia wakati wao kwa mambo ya kushangaza, mengi ambayo yamejazwa na ujuzi wa kishetani. [ Toleo katika nakala ya faili ya Chuo Kikuu cha Andrews ifuatavyo maneno "yaliyojazwa na ujuzi wa kishetani" kwenye ukurasa wa 2 wa Manuscript 124, 1901 , na imejumuishwa katika Manuscript Release 390: “Hawajajifunza mfano wa Nadabu na Abihu ambao walichanganya akili zao na matumizi ya divai na hawakuweza kutofautisha kati ya moto mtakatifu na wa kawaida. ] 17MR 237.1*_

_*Mungu hajatuweka kwenye kazi ya kuchapisha nadharia za kishetani. Kundi hili la wataalamu wa sanaa ya uandishi limewasilishwa kwangu likipinga njia ambazo kwa wakati wote zinapaswa kutumika kukutana na adui kwenye uwanja wake mwenyewe. Vitabu vyenye nadharia za uwongo vimeruhusiwa kutoka kwa idara inayodhibitiwa na Waadventista wa Sabato, wakati vitabu halisi ambavyo mameneja wangepaswa kuwa wenye kujitoa na bidii katika kuvisambaza kila mahali vimeachwa kwenye rafu pasipo kutumika. Wakati ukweli mtupu unachanganywa na kiwango cha udanganyifu wa kishetani, ni kwa jinsi gani Mungu anaweza kufanya kazi kwa maendeleo ya kusudi Lake? 17MR 237.2*_

_*Ukweli halisi kwamba sanaa ya uandishi wa kishetani imekuja kutoka kwa matbaa za idara ya Review na Herald, ni ushindi kwa nguvu za Shetani; kwani inaonekana inabeba sura (au idhini) ya idara, na adui atatumia ukweli huu kushawishi wengine kukubali jambo hili lisilofaa. Shetani sasa anafanya kazi "kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea" 17MR 238.1*_

_*Katika nafasi ya kushughulikia kazi ya kibiashara kama kitu cha umuhimu wa pili, wale walio na nafasi yenye dhamana hiyo wameichukulia kama ya umuhimu wa msingi. Vitabu ambavyo vinapaswa kusambazwa katika nyakati hizi za hatari vimewekwa kando mpaka kazi ya kidunia imalizike kwanza. Kundi la wataalamu wa sanaa ya uandishi ambalo Mungu amelihukumu (halikubali) hasa, limeruhusiwa kupokelewa. 17MR 238.2*_

_*Kuanzishwa kwa jambo hili kumeonyeshwa wazi kama njia bora zaidi ya kuwadhoofisha wanafunzi (wanagenzi). Inafunua ukosefu wa uamuzi kwa wale ambao wanahusiana na masuala haya. Wengine walio katika nafasi za uwajibikaji hawaongozwi na Roho Mtakatifu. Bwana huwaona kama mawakili wasio waaminifu wale ambao wamekubali kundi hili la wataalamu wa sanaa ya uandishi kuingia katika idara kwa ajili ya uchapishaji. Wanagenzi (wanafunzi) wanaofanya kazi katika idara wameachwa pasipo ulinzi na wachungaji wasio waaminifu. Mbegu za uovu zimekuwa zikipandwa ndani ya mioyo ya wanafunzi na katika mioyo ya wote ambao wameshughulikia sanaa (fasihi) hii - mbegu ambazo zitaota na kukua, "kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.” Kwa hivyo kosa litaendelea kukua. 17MR 238.3*_

_*Kwa nini upofu huu umekuwa juu ya wale ambao wamepewa majukumu mazito kuhusiana na nyumba zetu za uchapishaji? Kwanini wametembea kama vipofu? Kwa sababu wamepuuza nuru ambayo Mungu amewapa; kwa sababu hawajatii Maandiko wala shuhuda za onyo zilizotumwa kwao. Je! Wamefumbua macho yao, kwamba hawawezi kuona wala kuelewa maonyo yaliyotolewa katika Maandiko juu ya ujuzi (sayansi) wa uwongo? Je! Hawaoni umuhimu wa kuwa na utambuzi mzuri wa kiroho, ili waweze kuchagua mema na kukataa kila kitu ambacho kina tabia ya kuchanganya ufahamu? 17MR 238.4*_

_*Wale ambao wameshughulikia machapisho haya wameletwa kwa uhusiano wa karibu na mawakala wasioonekana, wa kishetani. Ni wangapi kati ya wale wanaofanya kazi juu ya jambo hili hatari lililowekwa mikononi mwao, wamechafuliwa! Ni wangapi, kwa sababu ya uhusiano wao na idara ya uchapishaji, wamejeruhiwa vibaya katika imani yao ya kidini! Ni mara ngapi imani imedhoofishwa kwa wasimamizi wa masilahi ya uchapishaji! Ni wangapi ambao imani yao imedhoofishwa kwa kupokea mawazo ya wasio waaminifu kwa ukweli, badala ya imani zao kuimarishwa kwa kupokea ujuzi ulioongezeka wa ujumbe wa mwisho wa rehema kutolewa kwa ulimwengu! 17MR 239.1*_

_*Ili kufanya kazi ambayo imefanywa, imekuwa muhimu kukodi wanafunzi wengi. Wanafunzi wanaopokelewa katika idara (ofisi) zetu za uchapishaji wanapaswa kupewa elimu makini na kamili katika kazi wanayotamani kujifunza. Na pia wanapaswa kupewa mafundisho kutoka kwa Neno la Mungu. Lakini katika elimu ya vijana wa kiume na wa kike ambao wameletwa idarani kumeonekana ulegevu, uzembe, na utendaji ovyo kwa kustaajabisha. 17MR 239.2*_

_*Bwana ametengwa na wengi kutoka kwa Idara kama asiye wa muhimu. Kila wakati uliowekwa kwa ajili ya mafundisho (maonyo) ya kitauwa (kidini) umekuwa mchache, na kana kwamba saa imeshikiliwa mkononi, ili wakati wa mwendelezo wa huduma hiyo uweze kuhesabiwa haswa. Wengine wameufanya muda uliotumiwa hivyo kama muda uliopotea sana. Je! tunaweza kustaajabu kuwa Bwana hapendezwi? Je! tunaweza kujiuliza kwa nini kuna uhaba wa kipato? Bwana hawezi kuwafanikisha wale wanaofanya kazi kama ile iliyofanywa. 17MR 239.3*_

_*Mabadiliko mengine yamefanywa. Mwaka jana kulikuwa na mkutano wa kushangaza zaidi wa uamsho katika Matbaa ya Pasifiki (Pacific Press), huko Oakland, ambapo wengi waliongolewa. Najua kwamba malaika wahudumu wa Mungu walikuwa pale. Lakini akili zetu hazijatulia. Mkutano huu umefanikishwa na kazi maalum, lakini  wafanyakazi wenyewe wasipolindwa siku hadi siku, Shetani atatafuta kupata nafasi yake ya kudhibiti, akiwaongoza katika njia za uwongo na kuwafanya wafanye kazi ngeni (isiyojulikana). 17MR 240.1*_

_*"Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako." Sheria imefanywa batili na wale ambao wamefuata kanuni mbaya ambazo zimeonyesha kazi kwa miaka kumi na miwili iliyopita. Wakati mambo haya yalipowasilishwa mbele yangu huko Australia, sura yote ya tatu ya Zakaria ilionyeshwa mbele yangu. Maneno haya yalirudiwa: "Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?” 17MR 240.2*_

_*Shetani alikuwa akituhumu Israeli waliorudi nyuma. Vivyo hivyo anakusudia kulenga kwenye hatua zisizo na misingi na haki za wale ambao wamekuwa na nuru kubwa katika siku hizi za mwisho. Anaona kwa hamu kurudi nyuma kwa wale ambao wamewekwa katika kusudi kuu la kazi - watu ambao kwa njia ya mawasiliano wamearifiwa kuwa hawakuwa kwenye nafasi na wasiofaa katika kuiwakilisha sauti ya mwenyekiti wa Jimbo Kuu kama sauti ya Mungu. Kwa miaka mingi haijawa hivi, na sasa haipo hivi; wala haitakuwa hivyo tena, isipokuwa kuwe na matengenezo kamili. 17MR 240.3*_
 
_*Baada ya Shetani kuwaongoza watu katika nafasi mbaya, anasimama mkono wa kulia wa malaika kama adui wa mwanadamu, kupinga kila juhudi iliyofanywa kuokoa watu walionunuliwa kwa damu ya Mwanakondoo wa Mungu. Ibilisi huwatesa wale ambao amesababisha watende dhambi. Yeye ni mshitaki wa ndugu. Mchana na usiku anawashutumu mbele za Mungu. Hii ndio kazi yake maalum. 17MR 241.1*_

_*Kupotoshwa kwa kanuni sahihi ni uvunjaji wa sheria ya Mungu. Wale ambao kwa matendo yao wanapotosha kanuni kuu za sheria Yake takatifu wako chini ya hukumu, kwani haki ya Kristo haiwezi kufunika dhambi moja isiyoungamwa. Sheria imekuwa ikichukuliwa yenye umuhimu kidogo. "Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya." Lazima tutii sheria ya Mungu, ikiwa sisi ni waaminifu kwake na tunakubaliwa naye. 17MR 241.2*_

_*Hatua ya kwanza kuelekea utii ni kujichunguza katika mwangaza wa sheria, hivyo kugundua adhabu ya uasi. Wale watu wa Mungu ambao hawatakasi nafsi zao kwa kuja kwenye nuru iliyo wazi zaidi na bado i wazi ni kemeo (au aibu) kwa kusudi Lake tukufu. Mara nyingi wale wanaopaswa kudumu wakweli na waaminifu kwa Amri hawafai kwa Mungu, kwa sababu katika haki Yake hawezi kuvumilia dhambi wanazozishikilia-dhambi ambazo sio tu zinawaongoza kwenye njia za uwongo lakini zinawasababisha wengine pia kupotoshwa (kutanga mbali/ kupotea njia). 17MR 241.3*_

_*Soma tena kwa uangalifu mafungu haya mawili: "Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?” Yoshua alikuwa mwakilishi wa watu wasio kamilifu, wenye dhambi, wale ambao walikuwa wamechafuliwa na dhambi. Shetani alimshtaki Yoshua kuwa mhalifu. Je! Ni nini basi tumaini la pekee la watu wa Mungu katika kukosa tabia ya Kikristo? tumaini lao pekee ni kuongoka, kutubu kwa Mungu, na imani katika Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye amefanywa kwetu haki na utakaso. Mbinguni Joshua alihesabiwa  mdhambi aliyehesabiwa haki. 17MR 241.4*_

_*Kisha, hapa, inakuja kazi ya Mkombozi. Shetani alisimama kando ya malaika kama adui, kumshtaki Yoshua kama muasi wa sheria. Malaika huyu, ambaye ni Mwokozi wetu, alionekana kwa Yohana wa ufunuo na alioneshwa kama amesimama katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu, amevikwa vazi hadi miguuni, na kujifunga kifuani na mshipi wa dhahabu. Kristo anawakilishwa katika huduma halisi kwa watu wake, kama ilivyokuwa kwa Yoshua katika siku ya upatanisho kwa niaba ya wana wa Israeli. 17MR 242.1*_

_*Kama vile katika wakati huo Shetani alionesha juu ya unajisi wa watu wa Mungu na kuridhika katika kupungua kwao, ndivyo anavyofanya sasa. Yoshua alishtakiwa kama mwenye dhambi; lakini Yesu Kristo, Mbeba-Dhambi, Mbadala kwa mkosaji, ambaye mifano yote inaelekezwa kwake, hawezi kushtakiwa hivi. Yeye ndiye anayechukua dhambi ya mwenye kutubu, akiamini ni mvunja sheria. Inasikitisha kiasi gani kwamba mawakala wa kibinadamu, kwa kupungua kwao kiroho, humfanya Shetani awashutumu kuwa hawafai! - Manuscript 124, 1901 . 17MR 242.2*_

_*Miliki ya Ellen G. White*_ 

_*Washington, DC,*_

_*Julai 9, 1987.*_

_*Maandishi yote.*_

Ujumbe wa kutisha sana huu kwa wahusika hasa wahariri katika viwanda vya uchapaji vya kanisa la MUNGU la SDA . Machapisho ya krismasi, siku kuu za mwaka mpya, mikesha ya mwaka mpya, vitabu vya nadharia vya watu binafsi visivyo na ujumbe wetu wa wakati huu, na mengineyo yote yaliyojaa majisifu ya dunia hii, Ni MACHAPISHO YA KISHETANI. Hatuyahitaji sisi watu wa MUNGU maana yamejaa upotoshaji mkubwa.

No comments