mafunzo ya watu wazima leo 29
LESONI, JANUARI 29
JIFUNZE ZAIDI:
“Moyo wa baba wa kibinadamu humwonea sana shauku mwanawe. Hutazama katika uso wa mwanawe mdogo, na hutetemeka anapowazia uwepo wa hatari dhidi ya maisha yake. Hutamani kumkinga mpendwa wake dhidi ya nguvu za Shetani, kumzuia asingiie katika majaribu na migogoro. Mungu alimtoa Mwana Wake wa pekee ili kukabiliana na mgogoro mkubwa zaidi na hatari, wa kutisha zaidi, ili njia ya maisha iwe ya uhakika kwa ajili ya watoto wetu wadogo. ‘Huu ndiyo upendo.’ Ajabia, Ee mbingu! Na shangaa, Ee dunia!” —Ellen G. White, The Desire of Ages, uk. 49.
“Kristo ndiye aliyekubali kutimiza masharti yaliyokuwa ya lazima kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Hakuna malaika, hakuna, mwanadamu, aliyeweza kutosheleza kwa ajili ya kazi hii kuu iliyopaswa kufanywa. Mwana wa Adamu pekee ilimpasa kuinuliwa juu; kwa kuwa asili isiyo na kikomo pekee ndiyo ingeweza kutekeleza mchakato wa ukombozi. Kristo alikubali kujiunganisha na wasiokuwa waaminifu na wenye dhambi, kushiriki asili ya mwanadamu, kutoa damu Yake Mwenyewe, na kuitoa nafsi Yake iwe kafara ya dhambi. Katika mashauri ya mbinguni, hatia ya mwanadamu ilipimwa, hasira kwa ajili ya dhambi ilikadiriwa, na bado Kristo alitangaza uamuzi Wake kuwa angejitwisha jukumu la kutimiza masharti ambayo kwayo tumaini lingepatikana kwa ajili ya kizazi kilichoanguka.” —Ellen G. White, The Signs of the Times, March 5, 1896.
MASWALI YA KUJADILI:
1. Kama tulivyoona katika Isaya 11, Bwana aliwasilisha awamu zote mbili za ujio wa Kristo katika picha moja. Ukweli huu unaweza kusaidia kuonesha, angalau kwa kiasi fulani, kwa nini baadhi ya Wayahudi walimkataa Kristo wakati wa ujio Wake wa kwanza, kwa sababu walitegemea afanye mambo ambayo yatatokea tu wakati wa Ujio Wake wa Pili. Jambo hili linatuambia nini kuhusu jinsi ilivyo muhimu kuwa na uelewa sahihi wa asili ya ujio wa Kristo? Kwa jinsi gani mawazo potofu, kwa mfano, kuhusu ujio Wake wa pili huwaandaa watu kwa ajili ya udanganyifu mkuu wa siku za mwisho wa Shetani? (Tazama Ellen G. White, The Great Controversy, sura ya 39.)
Muhtasari: Katika siku za Isaya, ambaye jina lake humaanisha “Wokovu wa Bwana,” Mungu aliahidi watu Wake waliosalia wokovu kutoka katika uonevu uliokuwa unawajia kama matokeo ya uasi wa taifa. Unabii huu wa tumaini ulitimizwa na Yesu, ambaye jina Lake humaanisha “Bwana ni wokovu.”
Post a Comment