amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Ijumaa 29/01/2021
*PUMZIKO LA MKRISTO*
*Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.* Mathayo 11:29
📝 Wewe [Addie Walling] wewe ni sawa kwangu na mtoto wangu mwenyewe. Nimefanya kwako kwa miaka, tangu ukiwa na umri wa miaka sita, majukumu ya mama. Umekuwa sehemu ya maisha yangu, sehemu yangu, na ikiwa una shida, ukiwa na mahitaji, ikiwa unahitaji fedha, nategemea uje kwangu kana kwamba mimi ni mama yako.
📝 Natumaini kwamba kusudi langu la kuwaasili [Addie na May Walling] kama watoto wangu litathibitika —ambayo ni kuwaona wote mkiwa wanawake wenye manufaa, watoto wa Mungu mkijenga tabia kwa ajili ya makao ambayo Yesu ameenda kuandaa kwa ajili ya wale wampendao. Ninatamani sana mfanye hili kuwa lengo, kusudi na mnachohangaikia maishani mwenu. Huku kujenga tabia ndio kazi kubwa kuliko zote. Siyo kazi ambayo hukoma katika maisha haya, bali itakayokuwa na athari kwa maisha yajayo.
📝 Mnayofanikiwa kufanya hapa kupitia wema na neema ya Kristo yatadumu kwa vizazi vya milele, na nimenuia kwamba msiwe katika kiwango cha chini. “Mjifunze kwangu,” anasema Mwalimu wa Walimu, “Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: nanyi mtapata raha nafsini mwenu.” Amani atoayo Kristo kamwe, kamwe haiwezi kuchangamana na huzuni ndani yake...
📝 Uwe mwenye busara na kukesha kwa maombi. Ujichunguze kwa makini na kufanya kazi ya dhati. Kuwa mwaminifu. Mara zote hisi kwamba upo katika uwepo wa Mungu na malaika watakatifu, Bwana anapaswa kupendezwa na kuheshimiwa na kutukuzwa...
🔘 *Addie, fanya kusudi lako kuwa mwanamke mwenye tabia njema, Mkristo wa kweli. Uwe na kweli moyoni. Nataka ujue wewe mwenyewe ujue uthamani wa upendo wa Mwokozi. Ikiwa Yesu atakaa ndani yako, tumaini la utukufu, kwa hakika utamdhihirisha Kristo kwa kuzungumza Habari zake; ikiwa amani yake ipo moyoni mwako kwa hakika utaonesha pia katika maneno na katika matendo yako. Jiamini mwenyewe na kuwa mnyenyekevu. Usiwe mwepesi kusema, bali mwenye staha; kamwe usijisifu, bali fikiri kidogo na kidogo kuhusu nafsi, na kusema kidogo kuhusu nafsi, na kumtwika Yesu mizigo yako yote. Bwana na akusaidie kuupata uzima wa milele.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment