unabii sehemu ya 5,PEMBE NDOGO
PEMBE NDOGO.
[Unabii :sehemu ya Tano]
Danieli 7:8
👉🏻Nikaziangalia pembe zake, natazama pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza ZIKANG'OLEWA kabisa, natazama katika pembe hiyo mlikuwa na macho, kama macho ya mwanadamu , na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
PEMBE NDOGO NI NINI??
Danieli 7:20,24
👉🏻Na ile pembe nyingine iliyozuka ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu, yaani pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
Danieli 7:24
👉🏻Na mwingine ataondoka baada ya hao, naye atakuwa mbali na hao wa kwanza, naye atawashusha wafalme watatu.
Kama tulivyokwishaona katika masomo yaliyotangulia, biblia ikifafanua yenyewe na kutueleza kuwa, 👇🏻👇🏻👇🏻
Pembe inawakilisha MFALME
Pembe tatu huwakilisha WAFALME WATATU.
Danieli 7:21,25
👉🏻Nikatazama, na pembe hiyo ilifanya vita na watakatifu , IKAWASHINDA.
👉🏻Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake aliye juu, naye ataazimu kubadili majira na sheria, nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati na nyakati mbili na nusu wakati.
Sasa mpenzi msomaji! Tuangalie kwanza sifa za hii Pembe Ndogo iliyozuka katikati ya zile pembe kumi zilizokuwa kwa yule mnyama wa nne mwenye kutisha mno na hii pembe ndogo ilipozuka tu ikazing'oa kwa haraka pembe tatu katika zile pembe kumi, na hivyo zikabaki pembe saba.
SIFA ZA PEMBE NDOGO ILIYOZUKA.
...................................................................
1. Ilizuka kati ya zili pembe kumi(yani ilitokea katikati ya wafalme kumi)
2. Iling'oa pembe tatu wakati inazuka(yani iliwaondoa wafalme watatu)
3. Ilinena maneno kinyume chake Aliye Juu(Aliye Juu ni MUNGU )Hivyo hii pembe ndogo ilimkufuru MUNGU Muumbaji.
4. Hii pembe ndogo ilifanya vita na watakatifu ikawashinda.
5. Itatawala kwa nyakati tatu na nusu,yani kwa miaka 1260.
6. Iliazimu kubadili majira na sheria
7. Itakuwa mbali na wafalme wa kwanza kutawala(itakuwa tofauti)
👉🏻 Yani falme zote zilizotangulia, hazikujaribu kubadili majira na sheria, hazikupambana na watakatifu wala kumkufuru Mungu, lakini hii pembe ndogo yenye macho na mdomo lakini isiyo na masikio ndiyo yenye kiburi na dharau dhidi ya Mungu. Ndo sababu wahubiri wengi wameihubiri hii pembe ndogo lakini haisikii, maana haina masikio🤔.
Sasa tuangalie, UNABII WA PEMBE NDOGO UNATIMIZWA NA NANI??
..........................................................................
(a) Pembe ndogo ilizuka kati ya zile pembe kumi au falme kumi, yani ilitokea katikati ya wafalme kumi.
👉🏻 Mpendwa, Rafiki, Tambuwa kuanzia sasa kuwa ile pembe ndogo ni mwendelezo wa Falme ile ya nne ya utawala wa romapagani, Hivyo mnyama wa nne yani ufalme wa romapagani haukufa/kukoma, bali ufalme huu uliendelea katika mtindo tofauti.
Je ni nani aliyeinuka baada ya ufalme wa rumi pagani kuanza kupoteza nguvu zake kisiasa???
👉🏻kwanza kabisa, hebu wanahistoria katika vitabu vyao watuambie👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
Katika kitabu cha Alexander Flick: THE RIZE OF THE MEDIAEVAL CHURCH. (New York:Franklin 1959) p. 150
Anasema:👉🏻Katika mabaki ya Rumi ya kisiasa, kuliinuka Taasisi ya kidini katika sura ya Taasisi mashuhuri, ijulikanayo kama kanisa la Rumi/Roma.
Kwa hakika wakati nusu ya magharibi ya himaya ya rumi ilipoangushwa na makabila ya kijerumani, Askofu wa Roma aliinuka na akawa kiongozi mashuhuri upande ule wa magharibi, na mda sio mrefu akawa anatekeleza sio tu MAMLAKA YA KIROHO BALI PIA YA KISIASA
Yani kwa haraka bila mashaka huyu mwanahistoria anatuambia kuwa pembe ndogo yenye macho kama macho ya mwanadamu na kanwa lililonena maneno makuu ya kumkufuru MUNGU ni UFALME WA KIDINI WA ROMA.
👉🏻Hapa hatupepesi macho, tunaongea na kujifunza mambo halisi yaliyopo katikati yetu.
Roma ya kidini ndiye pembe ndogo , BIBLIA inayo majibu ya wazi kumuhusu huyu pembe ndogo aliyenena maneno ya makufuru.
Askofu Mkuu wa Roma ya kidini(Pope) anayo mamlaka ya kidini/kiroho na pia anayo mamlaka ya kisiasa.
Wafuasi wa papa wanalijuwa hili na hawawezi kulibishia.
👉🏻hebu tuangalie kitabu kingine cha mwanahistoria wa tawala za dunia, ndugu👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
ADOLF HAMARK,
WHAT IS CHRISTIANITY ???
(New York :Putnam ,1901, uk 270
Anasema👇🏻👇🏻👇🏻
Kanisa la rumi kwa siri lilijichomeka mahali pa iliyokuwa himaya ya rumi ya kipagani, ambayo kweli ni muendelezo wa himaya hiyo. Ukweli ni kwamba himaya ya Rumi haikutoweka, inaendelea katika mtindo tofauti.
Rafiki, ndugu yangu msomaji, je wajuwa kuwa pembe ndogo ni ni mamlaka kubwa ya kidini duniani? Ndiyo ni mamlaka kubwa ya kidini duniani iliyoonea kila kona ya dunia, hata nchi zilizokuwa zinaikataa, sasa zinaikaribisha mamlaka hii kufanya nayo kazi na hata kuabudu nayo pamoja. Hivyo tunaona kuwa unabii wa pembe ndogo unatimizwa na kanisa la roma ya kidini. Mambo haya hata wao wanayajuwa vizuri mno. Huu ni ukweli usiopingika, hata ukiupinga unajisumbuwa maana unapambana na mwenye ukweli huu aliyetufunulia Aliye Juu, unabii wa MUNGU lazima utimie tu, upende usipende, neno la MUNGU ni kama mvua😅😅. Ufalme huu wa kidini unaungwa mkono duniani kote na unafanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wanasiasa wa dunia hii nini cha kufanya na nini wasifanye, kama vilevile yule mwanahistoria alivyoandika katika kitabu chake kuwa kiongozi wake mkuu anayo mamlaka ya kiroho na kisiasa.
PEMBE NDOGO(ufalme wa roma ya kidini) ULING'OA MATAIFA MATATU, HADI LEO HAYAPO.
👉🏻Wakati roma ya kidini ilipokuwa ikiinuka kuchukuwa utawala wa dunia, ilipingwa vikali na mataifa matatu yaliyokuwepo wakati huo, yani waostrogothi, waheruli na wavandali. Majeshi ya rumipagani yalishirikiana na mamlaka hii ya kidini, yalipigana vita dhidi ya hayo mataifa yaliyoipinga roma ya kidini na kuyashinda kabisa na kuyafuta hayo mataifa katika ramani ya ulaya, na mnamo mwaka wa 538AD roma ya kidini ilianza kutawala rasmi. Askofu mkuu (pope) wa roma akawa ndiye kiongozi wa dunia.
Mpendwa msomaji, kumbuka hii pembe ndogo ndiyo itakayokamilisha huu unabii, na baada ya hapo YESU atarudi duniani kuwachukua waliomshinda huyu mnyama na sanamu yake. Pambano bado linaendelea ndugu mpendwa, halijafikia mwisho, usidanganywe na mapambio ya uongo eti "Mbinguni ni tambarare" kuna vikwazo njiani tena njia imejaa miiba na fujo na njia ina paruza. Shikilia mkono wa MUNGU tu na usiuachie. Kama bado hujafanya maamuzi ya kumkimbilia YESU akuokoe, sasa ndiyo wakati wako. Siku ya wokovu wako ni leo, kesho siyo yako.
Mpendwa, Endelea kufatilia sehemu ya sita ya hii pembe ndogo.
BWANA Awabariki🙏🏻
Post a Comment