unabii sehemu ya 3,siku za mwisho zimefika

UNABII:Sehemu ya Tatu.

MNYAMA CHUI
..........................

Danieli 7:6
Kisha nikatazama na kumbe, mnyama mwingine kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege, mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne, akapewa mamlaka.

👉🏻Mnyama wa tatu chui anawakilisha utawala wa tatu ulioitawala dunia.
👉🏻Utawala huu ulianza kutawala mwaka 331bc hadi 168bc.
👉🏻Chui anawakilisha utawala wa wayunani/wagiriki.
👉🏻Mabawa manne huwakilisha nguvu na pia kasi na uhodari zaidi wa kivita.
👉🏻Kiongozi mkuu wa utawala huu aliitwa Alexander Mkuu.
👉🏻Vichwa vinne huonyesha mgawanyiko wa huu utawala , mgawanyiko uliotokea baada ya Alexander kufa.

Alexander alianza kutawala dunia akiwa na miaka 20, alianza kutawala makedonia na akadhamilia kuitawala dunia yte ya siku zake. Mwaka 338bc Baba yake mfalme filipo alifanikiwa kuunganisha sehemu kubwa zaidi ya uyunani kuwa sehemu ya Utawala wake.

Mwaka 334bc utawala huu ulikabiliana na majeshi ya waajemi na kuyashinda. Alexander akiwa na askari wa vita 35000 aliyashinda majeshi ya waajemi yenye askari wengi kuliko askari wa Alexander . Alexander aliiteka ngome ya dario mmedi na baada ya hpo alimfatilia na mfalme wa uajemi na kumshinda mnamo mwaka 331bc. Akiwa na umri wa miaka 33 Alexander alikufa sababu ya ulevi.

👉🏻Baada ya kifo chake mfalme Alexander mkuu, majemadari wake walianza kugombana kuhusu ni yupi awe mfalme. Huu ugomvi ulipelekea utawala wa wayunani kugawanyika katika majimbo madogo madogo manne.

👉🏻Majemedari wakuu wa Alexander walikuwa ni:

👉🏻Ptolemy
👉🏻Seleukus
👉🏻Lysimachus
👉🏻Cassander

majimbo manne waliyogawana ni haya👇🏻👇🏻👇🏻

Utawala wa Ptolemy 👇🏻👇🏻
misri, palestina, na shamu kusini.

utawala wa seleuchus👇🏻👇🏻
Asia , ashuru, shamu na india

utawala wa Lysimachus👇🏻👇🏻👇🏻
thrakia na sehemu za asia ndogo

Utawala wa Cassander👇🏻👇🏻👇🏻
makedonia na ugiriki.

👉🏻Hatimaye majimbo haya yalianza kudhoofika taratibu na kwa hakika, na baadaye rumi ikaanza kuyatawala hatua kwa hatua.

Huo ukawa ni mwisho wa utawala wa wayunani ambao ni sawa na sanamu ya ndoto ya nebukadreza. Danieli 2:39.

No comments