amka na Bwana leo 27
*KESHA LA ASUBUHI*
Jumatano 27/01/2021
*KUFIKIA MAPATANO*
Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. *2Wakorintho 1:10*
▶️Usiku uliopita nilikuwa kana kwamba nimesimama mbele ya idadi kubwa ya watu ambao hawakuwa wamoja. Mmoja alisimama nyuma wakati mwingine alitamani kwenda mbele. Hawakuwa wamesimama katika kuungana mmoja na mwingine. Niliona kiumbe wa kimbingu akitokea mbele yao, na kumsikia akisema; “Njooni katika mapatano! Hakuna anayepigana vita atakavyo yeye mwenyewe. Bwana wa makusanyiko anasema, Pataneni!”
▶️Baada ya hili, sikusinzia tena. Sikujua kama katika mkutano huu ndugu zetu walikuwa katika mapatano. Ni vigumu sana mara nyingi kwa kundi kubwa la watenda kazi kuwa katika kupatana mmoja na mwingine; lakini kila mmoja anapaswa kufikia mapatano, na kujaza nafasi yake aliochaguliwa. Mungu na awasaidie watumishi wake kufanya hili, ni ombi langu.
▶️Ingawa yawezekana wengine walifuata njia zao wenyewe kwa muda, inawezekana kwao kurudi, na kufika katika mapatano. Bwana huona kwamba si vizuri sana kwa watoto wake kuruhusiwa kufanya watakavyo, na kukataa kuungana na ndugu zao waonao mambo kwa namna fulani tofauti na wanavyoweza kuyaona wao.
▶️Kuna wengine ambao hawaitikii mwaliko kwa sababu ya njia yao wenyewe, na kuja katika mapatano na njia ya Mungu. Wanapendelea kufuata njia waliojichagulia wenyewe. Wale wanatamani kufanya hivyo, wana fursa ya kuendelea kutembea katika njia yao isiyo wakfu, bali mwisho wa hiyo njia ni huzuni na uharibifu.
▶️Mungu ana watu aliowachagua ambao atawatumia katika kazi yake kadiri watakavyoruhusu kutumiwa kulingana na mapenzi yake mema. Kamwe hawezi kumtumia mtu anayetaka kumnyenyekeza mtu mwingine. Jinyenyekezeni, ndugu Mkifanya hivi, inawezekana kwa malaika watakatifu kuwasiliana nanyi, na kuwaweka katika mahali palipo na manufaa. Kisha uzoefu wenu, badala ya kuwa na kasoro, utajazwa kwa furaha. Tafuteni kujihusisha wenyewe katika mapatano na maongozi ya Mungu, na kisha mtakuwa wenye kuongozwa na Roho Mtakatifu.
▶️Bwana anakuja. Mwisho wa mambo yote umefika. Umebakia muda kidogo tu kwa ajili ya kujenga tabia.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment