mafunzo ya watu wazima leo 27

LESONI, JANUARI 27

SOMO: MZIZI NA TAWI KWA PAMOJA (ISAYA 11)



Ni nani “chipukizi” linalotoka katika “shina la Yese” katika Isaya 11:1? Tazama pia Zek. 3:8; Zek. 6:12.

Isaya 11:1 huchukua picha ya mti ulioangushwa katika Isaya 10:33, 34. “shina la Yese” huwakilisha wazo kuwa ufalme wa Daudi (mwana wa Yese) ungepoteza mamlaka yake (Dan. 4:10—17) Lakini "chipukizi/tawi" lingechipuka kutoka katika “shina” ambalo linaonekana kama limekufa; yaani, mtawala ni mzao wa Daudi. 



Kwa nini mtawala mpya ambaye ni mzao wa Daudi aitwe pia “mzizi wa Yese” (Isa. 11:10)? Je, jambo hili linamaanisha nini? Ufu. 22:16.

Maelezo haya yanamstahili Yesu Kristo peke yake, ambaye Yeye kwa pamoja ni “Shina na Mzao wa Daudi” (Ufu. 22:16). Kristo alitoka katika ukoo wa Daudi (Luka 3:23—31), aliyekuwa mwana wa Adamu, aliyekuwa “mwana wa Mungu” (Luka 3:38) kwa maana ya kwamba Kristo alimuumba (tazama Yohana 1:1—3, 14). Kwa hiyo, Kristo alikuwa chimbuko la Daudi, pia alikuwa mzao wake! 



Ni kwa njia zipi mtawala mpya aliye mzao wa Daudi anabadili madhara ya dhambi na uasi? Isaya 11.

Anafikiri na anatenda kulingana na mapenzi ya Bwana, anahukumu kwa haki, anawaadhibu waovu, na analeta amani. Atakaposhika madaraka, Bwana atawarudisha, atawajenga upya, na atawaunganisha waaminifu waliosalia katika Israeli na Yuda (linganisha na Isa. 10:20—22). Kutakuwepo na ufalme imara mmoja ulioungana kama ilivyokuwa katika siku za Daudi, aliyewashinda Wafilisti na watu wengine. Lakini Mtawala Mpya atakuwa mkuu zaidi kuliko Daudi kwa maana kwamba atarudisha amani kama ilivyokuwa wakati wa uumbaji wenyewe: Wanyama wakali hawatakula nyama tena, na wataishi kwa amani na wanyama ambao walikuwa wanawala hapo awali (Isa. 11:6—9).



Je, Isaya 11 inazungumzia kuhusu ujio wa Kristo wa kwanza tu, ujio wa pili, au vyote pamoja? Pitia unabii huo ili kugundua ni aya zipi zinazungumzia ujio upi.

Katika Isaya 11, matukio ya ujio wa kwanza na ujio wa pili yamewasilishwa kama tukio moja. Matukio yote mawili yamefungwa pamoja, kwa sababu yote mawili ni sehemu mbili za kitu kimoja kizima, kama pande mbili za ubao ulio bapa. Mpango wa wokovu, ili ukamilishwe, unahitaji matukio yote mawili ya ujio wa Kristo: wa Kwanza, ambao umeshatokea tayari; na wa Pili, ambao tunausubiri kama ukamilisho wa matumaini yetu yote kama Wakristo. 



Ni jambo gani ambalo Kristo alilitimiza wakati wa ujio wa kwanza ambalo linatupatia uhakika kamili kuhusu Ujio wa Pili? Ni nini kusudi la Ujio wa Kwanza ikiwa hauishii katika Ujio wa Pili?

No comments