Mjoli katika Biblia
Yesu juu! Wajoli, nini maana ya Mjoli/Wajoli? Ndugu wengi katika Kristo wanasoma au kusikia neno mjoli/wajoli bila kujua maana yake nini, leo jua kuwa, Mjoli ni mtumishi, kibiblia tunaona katika Wafilipi 4:3. "Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami..." Tunaona utumizi wa neno mjoli, pia katika Ufunuo 22:9 "Naye akaniambia, angalia usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wandugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu." Chamsingi tunaona neno mjoli limetumika kama mtumwa au mtumishi, hivyo tunaposema wajoli wa Bwana twamaanisha WATUMWA /WATUMISHI WA BWANA. Mungu akubariki mjoli mwenzangu songa mbele kumtumikia BWANA Usitishwe na kelele za adui, MUNGU YU UPANDE WAKO ILI KUKUSAIDIA KIROHO NA KIMWILI. Amen.
AMEN AMEN MJOLI WA BWANA
ReplyDelete