amka na Bwana leo 23
KESHA LA ASUBUHI
Jumamosi 23/01/2021
*GAWIO LA KIMBINGU*
*Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.* Zaburi 60:4
💎 Hakikisha kwamba kweli imeandikwa katika bendera yako kwa nyakati zote na mahali pote. Kama taifa Wayahudi walikataa kumpokea Kristo. Alikuwa amewaongoza katika safari, kama kiongozi wao asiyeonekana na asiye na kikomo. Alikuwa amewaambia mapenzi yake, lakini katika jaribio walimkataa, Yeye Aliye tumaini lao pekee, wokovu wao pekee, naye Mungu aliwakataa.
💎 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Kwa wote wanaopokea na kutii masharti, vipawa vya Mungu hutiririka kwa uthabiti, pasipo kughairi, bila kubatilisha. Mungu ametoa vipawa vyake kwa mwanadamu ili kutumiwa, si kulingana na urithi, au mawazo ya ubunifu, si kulingana na msukumo au mwelekeo wa asili, bali kulingana na mapenzi yake...
💎 Wale waliomcha Mungu walipaswa kufikiri wao wenyewe. Hawakupaswa kuacha watu wengine wafikiri kwa ajili yao. Akili zao hazikupaswa kuendelea kufungwa katika kanuni, nadharia, na mafundisho yasiyo sahihi. Kukosa kujua na maovu, uhalifu na vurugu, mateso katika maeneo ya juu, ni lazima vifunuliwe. Nuru ya uzima ilikuja katika ulimwengu huu kuangaza katikati ya giza la kimaadili. Injili ingeweza kuhubiriwa miongoni mwa maskini,wanaokandamizwa. Wale waliokuwa katika maisha ya chini wangepewa nafasi ya kuelewa sifa halisi zinazohitajika kwa ajili ya kuingia katika ufalme wa Mungu.
💎 Na leo watu wa hali ya chini wanahitajika kuchukua nafasi yao katika kutii agizo, “Songa mbele.” Kwa imani watakutana na magumu, bila kukubaliana na mabishano na sauti zisizo na maana za lugha za kukosa imani. Wanapaswa kusonga mbele toka kiwango kimoja cha mafanikio kwenda kingine, kwa kuomba kila mara, na kutendea kazi ile imani inayojibu maombi.
🔘 *Mawakala wa Mungu ni wengi! Bali wale waliohiari kufanya kazi kulingana na mpango wa Mungu wanajumuishwa katika maneno, "Maana si tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu” (1 Wakorintho 3:9). Watumishi wa Mungu wanapaswa kusonga mbele ili kwamba kusiwepo karama ya kiroho itakayopotea. Mapenzi yao yanapaswa kushikiliwa katika kutotumika kwa muda, na wakati wa Bwana utakapokuja, fimbo itachanua. Kazi itakuwa na sura gani hakuna awezaye kujua, lakini watumishi wa Mungu wanapaswa kuwa tayari kupambana wakati wowote, tayari kutambua njia na mapenzi ya kiongozi wao.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment