mafunzo ya watu wazima leo 10

LESONI, JANUARI 10

SOMO: HATARI KUTOKA KASKAZINI (ISA. 7:1—9)



Ni tatizo gani kubwa lilimkabili mfalme Ahazi mwanzoni mwa utawala wake? 2 Fal. 15:37, 38; 2 Fal. 16:5, 6; Isa. 7:1, 2.

Falme za Kaskazini mwa Israeli (Efraimu) na Shamu (Aramu) ziliungana dhidi ya nchi ndogo ya Yuda, iliyoko Kusini. Jambo hili lilitokea wakati Yuda ilipokuwa imedhoofishwa kwa mashambulizi ya Waedomi na Wafilisti. Wakati uliopita, Yuda ilipigana na Israeli, lakini umoja wa Israeli na Shamu ulikuwa wa hatari kubwa sana. 



Inaonekana Israeli na Shamu walitaka kuilazimisha Yuda ishirikiane nao ili waunde umoja dhidi ya utawala wenye nguvu kubwa wa Tiglath-pileser III wa Waashuru (aliyeitwa “Pulu” katika 2 Wafalme 15:19), aliyeendelea kuwa tishio kwao kwa sababu ya ufalme wake uliokuwa ukipanuka daima. Israeli na Shamu walikuwa wameweka pembeni migogoro ya siku nyingi kati yao kwa sababu ya hatari kubwa zaidi iliyowakabili. Ikiwa wangeishinda Yuda na kusimika mtawala aliye kibaraka wao pale (Isa. 7:5, 6), wangeweza kutumia rasilimali za Yuda na kunufaika na nguvu kazi ya watu wa Yuda. 



Suluhisho la Ahazi lilikuwa ni nini wakati ulimwengu wake ulipokuwa unasambaratika? 2 Wafalme 16:7—9, 2 Nya. 28:16.



Badala ya kutambua kuwa Mungu ndiye aliyekuwa rafiki pekee ambaye angeweza kumwokoa na kuiokoa nchi yake, Ahazi alijaribu kumfanya Tiglath-pleser III adui wa maadui zake, awe rafiki yake. Mfalme wa Kiashuru alilikubali kwa furaha ombi lake dhidi ya Shamu na Israeli. Siyo tu kuwa Tiglath-pileser alipokea rushwa kubwa kutoka kwa Ahazi, bali pia alipata kisingizio kizuri cha kuiteka Siria, na alifanya hivyo mara moja (2 Wafalme 16:9). Nguvu ya muungano wa Shamu na Israeli ilikwisha. Kwa muda mfupi, ilionekana kana kwamba Ahazi ameiokoa Yuda. 



Tendo hili kwa upande wa Ahazi, hata hivyo, halikuwa la kushangaza. Alikuwa mfalme mbaya kuliko wafalme wote wa Yuda waliomtangulia. (Tazama 2 Wafalme 16:3, 4; 2 Nyakati 28:2—4.) 



Tunaposoma na kuelewa vile Ahazi alivyokuwa, inaeleweka wazi kwa nini alitenda vile alivyotenda wakati wa hatari. Hapa kuna somo gani kwa ajili ya kila mmoja wetu binafsi? Ikiwa hatumtii Bwana sasa, ni jambo gani linatufanya tufikiri kuwa tutakuwa na imani ya kumtumaini wakati majaribu yatakapokuja? (Tazama Yakobo 2:22, Yer. 12:5.

No comments