amka na Bwana

*KESHA LA ASUBUHI* 

 *Jumapili 10/01/2021* 

*TIBA YA KUTOJALI*

" _Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."_ 
Warumi 1:16

▶️ Hakuna upungufu katika mpango wa Mungu wa ukombozi wa wanadamu. Kama injili siyo nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila mtu, si kwa sababu injili ina dosari, bali kwa sababu wanadamu si waumini wa kivitendo, wapokeaji wa kivitendo wa neema na haki ya Kristo... Waumini wa jina hawamchukulii Kristo kama Mwokozi wao binafsi, bali humfuata Yesu kwa mbali sana. Sababu moja ya ukosefu wa hii dini binafsi ni kwamba hawakufundishwa katika kanuni hizi muhimu.

▶️ Sababu nyingine ya hali ya kutojali na kutojihusisha katika kanisa letu ni kwamba washiriki vijana hawakufundishwa kwa uvumilivu na ustahimilivu namna ya kutenda kazi kama askari waaminifu katika jeshi la Kristo... 

▶️ Wengi wamepokea kweli pasipo kuzama kwa kina ili kuelewa kanuni zake za msingi, na inapopingwa, wanasahau hoja na ushahidi unaoitegemeza. Inapaswa isisitizwe kwa wote kwamba maarifa ya kweli ya kudumu yanaweza kupatikana tu kwa kazi ya dhati na nguvu ya ustahimilivu. Kama akili za watu zingeletwa katika nidhamu kwa kuchunguza sana Maandiko, wangekuwepo mamia ya walioongolewa katika kweli mahali penye mmoja tu leo... 

▶️ Wengi bado hawana utambuzi kama vile wapagani katika suala la namna ya mdhambi anavyoweza kuja kwa Mungu na kuhesabiwa haki mbele zake. Hawana cha kujitetea kwa ajili ya kutotambua kwao; kwa kuwa maneno yaliyovuviwa yanasema, “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). “Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa” (Mithali 9:10) 

▶️Uzoefu wa kidini usio na msingi katika Kristo peke yake hauna thamani .... Watu wenye uwezo wa kiakili wanahitaji uwasilisho wa wazi wa kiroho wa mpango wa wokovu. Hebu ukweli na uhalisia na nguvu yake uwasilishwe kwao. Kama hii haitashika usikivu wao na kuibua shauku yao, hawawezi kamwe kuwa na shauku katika mambo ya mbinguni ya kiungu. Katika kila kusanyiko kuna roho ambazo haziridhiki. Kila Sabato wanahitaji kusikia kitu cha wazi kikifafanua namna wanavyoweza kuokolewa, namna wanavyoweza kuwa Wakristo. Kitu cha muhimu kwao kujua ni, ni kwa namna gani mdhambi anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu?

No comments