mafunzo ya watu wazima leo 17

LESONI, JANUARI 17

SOMO: KUTIMIZWA KWA UNABII (ISA. 7:14—16)



Katika Isaya 7:14—16, Imanueli ni ishara ambayo imeshikamana na mtanziko mahsusi wa Ahazi: Kabla mtoto Imanueli hajawa mtu mzima wa kutosha kutofautisha vyakula vya aina mbalimbali, "nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa" (Isa. 7:16). Unabii huu unazungumzia nchi ya wafalme wa Shamu na Israeli ya kaskazini (tazama Isa. 7:1, 2, 4—9) na unarudia ahadi ya Mungu kuwa nguvu zao zitakwisha hivi karibuni. 



Kwa nini Isaya anasema kuwa mtoto mwanamume atapaswa kula "siagi na asali" ? Isa. 7:15.



Mazao na mashamba ya Yuda yangeharibiwa na Waashuru (Isa. 7:23—25). Hivyo watu, ikiwa ni pamoja na Imanueli wa Agano la Kale, bila kujali alikuwa ni nani (Isa. 7:14, 15), wangelazimika kurudia chakula cha watu wanaohamahama (Isa. 7:21, 22). Lakini ingawa wangekuwa maskini, wangekuwa na chakula cha kutosha kuwawezesha waishi. 



Ni lini unabii unaohusu Shamu na Israeli kaskazini ulitimizwa? 2 Fal. 15:29, 30; 2 Fal. 16:7—9; 1 Nya. 5:6, 26.



Unabii huu wa Isaya ulitolewa mnamo mwaka 734 K.K. Kama matokeo ya rushwa ya Ahazi, Tiglath-pileseri III alifanya jambo ambalo angelifanya kwa vyo vyote vile: Aliuvunja muungano wa kaskazini, aliishinda Galilaya na maeneo ya Yordani ya kaskazini mwa Israeli, aliwatawanya baadhi ya wakazi, na aliyabadilisha maeneo kuwa majimbo ya Ashuru (734—733 K.K.). Waisraeli waliosalia waliookolewa pale Hoshea, baada ya kumwua Mfalme wa Peka, alijisalimisha na kulipa ushuru. Mwaka 733 na 732 K.K. Tiglath-pileseri aliuteka mji wa Dameski, mji mkuu wa Shamu. Ndipo alipoifanya Shamu kuwa majimbo ya Ashuru. Hivyo, mwaka 732 ulipowadia, ndani ya miaka kama miwili hivi ya utabiri wa Isaya, Shamu na Israeli walikuwa wameshindwa kabisa, na wafalme wawili waliokuwa tishio kwa Ahazi wakawa wameishia hapo. 



Mara tu baada ya Shalmaneseri V kuchukua nafasi ya Tiglath-pileseri III katika mwaka 727 K.K., Mfalme Hoshea wa Israeli alijinyonga kisiasa kwa kuiasi Ashuru. Waashuru waliuteka mji mkuu wa Samaria mwaka 722 K.K. na kuhamishia maelfu ya Waisraeli Mesopotamia na Media, ambapo hatimaye walimezwa na wakazi wa maeneo mahalia na kupoteza utambulisho wao (tazama Isa. 7:8 —ndani ya miaka 65 Efraimu haikujulikana kabisa kama kundi la watu). Mungu alikuwa amesema kile ambacho kingetokea hata hivyo, bila msaada wa Waashuru.



Fikiria, kama ungekuwa unaishi katika ufalme wa kaskazini wakati mambo haya yote yalipotokea, ni kwa urahisi kiasi gani ungeweza kupoteza imani? Tunaweza kufanya nini, sasa, leo, kujizoeza kudumisha imani, ili kwamba wakati majanga yakija kesho, tuweze kubaki tukiwa imara? Tazama 1 Pet. 1:13—25.

No comments