KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 16 ADAIWA KUMUUA BINAMU YAKE KWA KUMCHINJA

KIJANA mmoja mwenye umri wa miaka 16 katika eneo la Embu nchini Kenya, anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo kwa tuhuma za kumuua binamu yake ambaye ni mtoto wa miaka minne, Brayden Mutwiri na kunywa damu yake kwa kile kinadhaniwa kuwa kitendo cha utoaji kafara kisha kuutupa mwili wa mtoto huyo mtoni.

Mwanafunzi huyo wa darasa la 8, juzi Jumatano aliwaongoza maofisa wa upelelezi nchini humo hadi katika Mto Thuci ambapo waliukuta mwili wa Mutwiri ukiwa ndani ya mto huo huku ukiwa umeharibika vibaya hata kushindwa kuutambua vizuri kwani umekaa ndani ya maji kwa wiki  nzima.

Mutwiri alipotea mwishoni mwa mwezi Desemba, mwaka jana 2020, nyumbani kwao Kavengero, Mbeere Kaskazini. Mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake walikamatwa Jumatatu na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Siakago kwa mahojiano baada kupatikana kwa taarifa kuwa anahusika na tukio.
#BinagoUPDATES

No comments