amka na Bwana leo 17
KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 17/01/2021
*KIPIMO CHA UKRISTO*
*Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.* Mathayo 5:13
🔰 Wale waliowekwa kwenye nafasi za dhamana sharti wawe na mamlaka ya kutenda, lakini hawapaswi kutumia mamlaka haya kama kigezo cha kukataa kusaidia wahitaji na wasio na msaada. Hayapaswi kutumika kukatisha tamaa au kukandamiza roho moja iliyo katika mahangaiko. Hebu wale waliopewa nafasi za mvuto wakumbuke kwamba Mungu anataka wabebe nia ya Kristo....
🔰 Uchaji Mungu wa kweli hupimwa kwa kazi iliyofanyika. Kukiri si kitu; cheo si kitu; tabia kama ya Kristo ni uthibitisho tunaopaswa kuonesha kwamba Mungu alimtuma mwana wake ulimwenguni. Wale wanaodai kuwa ni Wakristo, bali hawatendi kama ambavyo Kristo angetenda kama angekuwa katika nafasi zao, wanaathiri sana kazi ya Mungu. Wanamwakilisha vibaya Mwokozi wao, na wanasimama chini ya rangi bandia.
🔰 Mwanafunzi wa kweli, ambaye Yesu anakaa katika moyo wake, huonesha ulimwenguni upendo wa Yesu kwa wanadamu. Yeye ni mkono wa Mungu wa msaada. Mng’ao wa ustawi wa kiroho husisimua nafsi yake yote kadiri apokeavyo neema kutoka kwa Mwokozi ili kutoa kwa wengine...
🔰 Dini safi isiyo na waa sio hisia, bali utendaji wa kazi za upendo na rehema. Dini hii ni ya lazima kwa ustawi na furaha. Huingia katika hekalu lililochafuliwa la moyo, na kwa mjeledi hufukuza uvamizi wa dhambi. Ikitawala moyoni, huweka wakfu vyote kwa uwepo wake, ikiangazia moyo kwa mwali angavu wa Jua la Haki. Hufungua madirisha ya moyo kuelekea mbinguni, ikiruhusu mwanga wa upendo wa Mungu kuingia. Huleta amani na utulivu. Nguvu ya kimwili, kiakili, na kimaadili huongezeka, kwa sababu mazingira ya kimbingu, kama wakala tendaji aliye hai, huujaza moyo...
🔘 *Wakristo wanaposhindwa kumdhihirisha Kristo, wana manufaa gani? Je, wao si kama chumvi isiyo na ladha, "isiyofaa kitu"? Lakini wanapofunua katika maisha yao nguvu iokoayo ya kweli, roho dhaifu zenye mioyo migumu kwa sababu ya dhambi haziachwi zipotee katika upotovu. Kazi mjema huonekana; kwa kuwa kanuni hai za haki haziwezi kufichwa. Injili inayodhihirishwa kwa vitendo ni kama chumvi iliyo na ladha yake yote. Ina nguvu katika kuokoa roho.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment