Mafunzo ya watu wazima leo 15
LESONI, JANUARI 15
JIFUNZE ZAIDI:
" 'Jina Lake ataitwa Imanueli ... Mungu pamoja nasi.’ ‘Nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu’ inaoonekana ‘katika uso wa Yesu Kristo.’ Tangu milele na milele Bwana Yesu Kristo alikuwa mmoja na Baba; Alikuwa ‘sura ya Mungu,’ sura ya ukuu na utukufu Wake, ‘mng’ao wa utukufu Wake.’ Alikuja katika ulimwengu wetu ili kudhihirisha utukufu huu. Alikuja kudhihirisha nuru ya upendo wa Mungu katika dunia hii ambayo iko gizani, —ili kuwa ‘Mungu pamoja nasi.’ Kwa hiyo ilitabiriwa juu Yake kuwa, ‘Jina Lake ataitwa Imanueli' " —Ellen G. White, The Desire of Ages, uk. 19.
“Ingekuwa kwa faida ya ufalme wa Yuda kama Ahazi angeupokea ujumbe huu kama ujumbe uliotoka mbinguni. Lakini kwa kuchagua kutegemea mkono wa mwanadamu, alitafuta msaada kutoka kwa mpagani. Katika kutapatapa alituma ujumbe kwa Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru: ‘Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia' 2 Kings 16:7. Ombi liliambatana na zawadi nono kutoka katika hazina ya mfalme na kutoka katika ghala la hekalu" —Ellen G. White, Prophets and Kings, uk. 329.
MASWALI YA KUJADILI:
1. Unapokuwa katika mchakato wa kufanya uamuzi, je, ni sahihi kuomba ishara kutoka kwa Mungu? Ni hatari gani zinaweza kuambatana na mchakato kama huo?
2. Ni vizuri kupata msaada wa wanadamu, lakini unajuaje mipaka yake?
3. Mwandishi wa Kirusi, Leo Tolstoy, alimwandikia rafiki yake kuwa “mtu anapotambua kuwa kifo ni mwisho wa mambo yote, hivyo hakuna jambo baya zaidi kuliko kuishi.” Ufahamu wetu kuwa “Mungu yuko pamoja nasi” unajibuje kauli hii?
Muhtasari: Mungu alimleta Mfalme Ahazi katika mazingira ambayo alitakiwa kufanya maamuzi magumu: Kuamini au kutokuamini ndiyo hoja ya msingi hapa. Japokuwa Bwana alimpa ruhusa aombe ishara yo yote ambayo angeifikiria, Ahazi alikataa kumruhusu Mungu amwoneshe sababu kwa nini alipaswa kuamini. Badala yake, alichagua “rafiki” yake mfalme wa Ashuru. 🙏
Post a Comment