amka na Bwana leo 15

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA, JANUARI, 15, 2021
SOMO: MSAADA UMEAHIDIWA 

Je! neno langu si kama moto? asema BWANA! na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? 

Yeremia 23:29. 



Bwana anatamani watoto wake wafanye vizuri sehemu yao, na kuwa na amani wao kwa wao kupitia kwa Kristo, mtoa amani. Kristo anapokaa moyoni, uwezo wa nafsi katika ukamilifu wake hutenda kazi katika umoja na upatanifu. Mantiki ya kila mtu mkamilifu, na upendo, vikijua namna ya kufanya sehemu zake, hutenda kazi kwa pamoja kwa kuungana. Kama vile mfalme katika kiti chake cha enzi, haki hutawala utaratibu wote wa utendaji. 



Inawezekana kuwa kazi kubwa inahitajika katika kujenga tabia yako, kwamba wewe ni jiwe lisilo zuri ambalo lazima lisawazishwe na kulainishwa kabla halijawa tayari kujaza nafasi katika hekalu la Mungu. Usistaajabishwe ikiwa kwa nyundo na patasi Mungu atakata dosari zako za tabia, mpaka uwe umefaa kujaza nafasi aliyoandaa tayari kwa ajili yako. Hakuna mwanadamu awezaye kukamilisha kazi hii. Inaweza kufanywa na Mungu tu. Na uwe na hakika kwamba hatapiga nyundo yoyote bila manufaa. Kila pigo lake hupigwa kwa upendo, kwa ajili ya mema na furaha yako ya milele. Anaujua udhaifu wako, na anatenda kazi kuboresha, wala si kuharibu. 



Kwa nini tunageukia hekima ya kibinadamu kutoka katika hekima ya kiungu? Mungu huona tunavyomtendea pasipo heshima. Anajua kwamba katika ubinadamu hatutapata faraja katika huzuni yetu, na anatuhurumia kwa sababu tu wahitaji sana, japo hatutaki kumfanya msiri wetu, mbeba mizigo yetu. Huwaona wanadamu wakipuuza upendo na rehema iliyotolewa kwa ajili yao, naye husema kwa huzuni, "Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima" (Yohana 5:40) 



Kutokuamini kwetu ni fedheha kwake yeye aliyefanya mengi kwa ajili yetu. Kamwe hatawaacha wale wanaokuja kwake. Kwa masikini, nafsi izimiayo, iliyochoka kuutazama ubinadamu kisha tu kusalitiwa na kusahauliwa, Kristo anasema, “Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami” (Isaya 27:5). 



Kristo anatamani kusema kwa watu wake kama alivyosema kwa Israeli ya zamani, “Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana Mungu” (Ezekieli 16:14).

No comments