CHUCK NORRIS AKANUSHA TAARIFA ZILIZOZAGAA MITANDAONI
Msanii maarufu wa filamu Chuck Norris amelazimika kukanusha kutoshiriki katika vurugu zilizotokea wiki iliyopita katika jengo la bunge la seneti la Marekani- Capital Hill, baada ya picha ya mtu aliyefanana na yeye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii"
Baada ya maandamano hayo, picha hiyo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ya wafuasi wa Rais Donald Trump, ambao walishirikisha picha ya mtu huyo Chuck Norris ambaye sasa ana umri wa miaka 80"
Picha ya mwanaume huyo ambaye anafanana na Chuck Noris , ilisababisha mkanganyiko, huku wengi mtandaoni wakiamini nyota huyo wa filamu kweli alikuwa miongoni mwa watu waliosababisha vurugu katika Capital Hill."
#BinagoUPDATES
Post a Comment