mafunzo ya watu wazima leo 1

LESONI, FEBRUARI 1

SOMO: MJI MKUU ULIOPITA WA BABELI (ISA. 13:2—22)



Mwaka 626 K.K. Nabopolasa Mkaldayo aliirudishia Babeli utukufu kwa kujifanya mwenyewe kuwa mfalme wa Babeli, akaanzisha dola mpya Babeli, na akashiriki (akiwa na Waamedi) katika kuishinda Ashuru. Mwanawe, Nebuchadneza II, alikuwa mfalme aliyeteka Yuda na kuwachukua mateka watu wake. 



Mji wa Babeli uliishaje? Tazama Danieli 5.

Katika 539 K.K., wakati Koreshi Mwajemi alipoiteka Babeli kwa ajili ya Dola ya Waamedi na Waajemi (tazama Danieli 5), mji ulipoteza uhuru wake milele. Mwaka 482 K.K., Artashasta I alidhibiti kikatili uasi wa Babeli dhidi ya utawala wa Uajemi. Alibomoa sanamu ya Marduk, mungu mkuu, na kwa kiasi fulani alibomoa baadhi ya ngome na mahekalu. 



Aleksanda Mkuu aliiteka Babeli kutoka kwa waajemi mwaka 331 K.K. bila kupigana. Licha ya muda mfupi wa njozi yake ya kuifanya Babeli kuwa mji mkuu wa mashariki, mji ulidorora pole pole kwa karne kadhaa. Mpaka mwaka 198 B.K. Mrumi, Septimus Severus, aliukuta mji wa Babeli ukiwa umetelekezwa. Hivyo, mji mkuu ulifikia ukomo wake za eneo la Babeli ya zamani, lakini hawajaujenga mji kama ulivyokuwa. 



Anguko la Babeli, lililoelezwa katika Isaya 13, linawaweka huru wazaliwa wa Yakobo, waliokandamizwa na Babeli (Isa. 14:1—3) Tukio lililowezesha jambo hilo ni Koreshi kuishinda Babeli mwaka 539 K.K. Ingawa hakuuangamiza mji, huu ulikuwa mwanzo wa mwisho wa Babeli, na haukurudia tena kuwa tishio kwa watu wa Mungu. 



Isaya 13 huigiza kuanguka kwa Babeli kama matokeo ya hukumu ya Mungu. Wapiganaji wanaouteka mji ni mawakala wa Mungu (Isa. 13:2—5). Wakati wa hukumu unaitwa “siku ya BWANA” (Isa. 13:6, 9), na hasira ya Mungu ina nguvu nyingi kiasi cha kuathiri nyota, jua, mwezi, mbingu, na dunia (Isa. 13:10, 13). 



Linganisha na Waamuzi 5, ambapo wimbo wa Debora na Baraka unamwelezea Bwana akienda na dunia ikitetemeka na mvua ikinyesha kutoka mbinguni (Amu. 5:4). Waamuzi 5:20, 21 huonesha vitu vya asili, ikiwa ni pamoja na nyota, vikipambana na mkandamizaji kutoka nchi Za nje. Fikiria ikiwa mtu aliyeishi Babeli wakati utukufu wake ukiwa juu kabisa angesoma Isaya 13, hususani Isaya 13:19—22. Ni kwa kiwango gani maneno hayo yangeonekana ya kipumbavu na yasiyowezekana! 



Ni maelezo gani mengine ya kiunabii, ambayo yanaonekana kuwa ya kipumbavu na yasiyowezekana kwetu sasa? Kwa nini tutakuwa wapumbavu, hata hivyo, tukiyapuuza na kusema hayawezekani?

No comments