amka na Bwana leo 1

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, FEBRUARI, 1, 2021
SOMO: ANACHOKITARAJIA MUNGU

Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyekevu.... Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. 

Yakobo 4:6—10. 



Wakati Mungu anapowapatia watu majukumu, anawatarajia kutii sheria yake. Wanapaswa kutenda kwa haki, wakitambua ya kwamba Bwana hutazama wanavyoshughulika na wanadamu wenzao, na kwamba ataadhibu kila tendo lisilo haki na dhalimu. Mungu huwapatia wanadamu nafasi ya kuwa wamoja na Kristo na wamoja naye. Wale wanaotembea katika hofu ya Mungu, wakitafakari juu ya tabia yake, watakuwa kila siku zaidi na zaidi kama vile Kristo. Wale wanaochagua kutokumjua Mungu watakuwa wenye kujidai na kujionea fahari.



Kuna wengi wanaojivika kile wanachodhani kuwa heshima kubwa. Bali machoni pa Mungu ni wajinga. Hawajatazama katika kioo cha kiungu, na hawajui ni kwa jinsi gani kujidai kwao hudharauliwa machoni pa Mungu mtakatifu. Yeye atazamaye kwa ndani hudharau kujitosheleza kwao wenyewe. Wanaweza kuwa na vyeo vikubwa kanisani au duniani, lakini kadiri wanavyoendelea kumdharau Muumbaji wao, na kutafuta kuabudiwa, wana hatia mbele zake. 



Mungu hafurahii kuwaadhibu wale wanaotembea kinyume naye, wakitoa uwakilishi bandia wa tabia yake. Bali kama hawatatubu, wakati unakuja ambapo lazima wavune thawabu ya hakika ya matendo yao. 



Wale walioingia katika agano kumtumikia Mungu wanapaswa kuwa na hofu maisha yao yasije yakawa hayaoneshi tofauti kati ya kweli na uongo. Hawapaswi kugeuka upande kuendea njozi zisizofaa na ubunifu wa kibinadamu na sifa zisizostahili. Maisha ya wenye haki yatawaaibisha wale wanaokataa kutoa utii wao kwa Mungu.... Mungu huwaita watu wake kutembea mbele zake katika unyenyekevu wote. Anataka wafikie kiwango cha juu tena juu zaidi katika ufahamu wa kiroho. Anashikilia kila mvuto kuwaongoza wanadamu kurudi katika utii wao kwake.... 



Mungu hutafuta kuwaongoza wanadamu katika kujinyenyekesha. Anajaribu kuwaongoza kuweka miguu yao katika hatua za umisionari mkuu wa kitabibu. Bali Mkombozi mara nyingi hukatishwa tamaa na kusulubiwa upya na wale wanaojidai mno. 

No comments