KESHO TUTAMTAMBULISHA KOCHA MPYA PAMOJA NA WASAIDIZI WAKE WAWILI
"Tunatangaza mashindano mapya ya SIMBA INTER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu. Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021." - CEO Barbara Gonzalez
Kupitia mashindano haya Wanasimba watapata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya na kocha. Kuanzia kesho tutatangaza watu ambao tumewaongeza katika benchi la ufundi." - Msemaji wa klabu, Haji Manara
Kesho tutamtambulisha kocha mpya na wasaidizi wake wawili pamoja na benchi la ufundi ambao wataiongoza timu kwenye mashindano mbalimbali. Kupitia mashindano ya Simba Super Cup, tutawatambulisha wachezaji wetu wapya kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa." - Haji Manara
#NguvuMoja
#AnotherLeveL
#BinagoUPDATES
Post a Comment