amka na Bwana
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumamosi, 09/01/2021.
*MAVAZI MAZURI.*
*Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu. Isaya 52:1.*
Wakati wa usiku nilipitia katika uzoefu unaofanana na ule niliokuwa nao nikiwa Salamanca, New York, miaka miwili iliyopita. Nilipoamka toka katika usingizi wangu wa kwanza mfupi, mwanga ulionekana kunizunguka pande zote, chumba kilionekana kujazwa na malaika wa mbinguni. Roho wa Mungu alikuwa juu yangu, na moyo wangu ulijaa na kufurika. Ni upendo wa ajabu kiasi gani uliochoma ndani ya moyo wangu! Nilikuwa nikipaza sauti, *"Bwana Yesu, ninakupenda; Wewe wajua kwamba nakupenda. Baba yangu wa mbinguni, nakusifu kwa moyo wangu wote. ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele’ (Yohana 3:16). *"Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu (Mithali 4:18). Yesu, Mwokozi wangu, Mwakilishi wa Baba, ninaweka tumaini langu kwako.”*
Amani yangu ilikuwa kama mto, nilionekana kama niliyefungiwa ndani pamoja na Mungu, katika ushirika mtamu pamoja naye katika kutembea kwangu na saa za kulala. *Ni fadhila ya juu na takatifu kiasi gani niliyokuwa nayo katika pendo la Yesu, maisha yake na ulinzi wake.*
Ni kwa nini kanisa la Kristo lisiamke, na kuvalia mavazi yake mazuri! Kwa nini haliangazi? *Sababu kubwa ya Ukristo hafifu namna hiyo ni kwamba wale wanaodai kuiamini kweli wanamfahamu kidogo sana Kristo, na hivyo kuwa na utambuzi wa chini sana wa kile atakachokuwa kwao, na kile wanachoweza kuwa kwake. Tunazo kweli za dhati na nzito kuwahi kukabidhiwa kwa watu wenye miili ya kufa.*
Kama ingekuwa maneno yetu, mawazo yetu, matendo yetu ni safi sana na yenye kuadilisha, zaidi kulingana na imani takatifu tunayoikiri, tungetazama majukumu yetu katika namna ya tofauti. Yangeweza kuonekana ya dhati, na takatifu kwa uajabu ulioje! Tungekuwa na utambuzi wa kina juu ya wajibu wetu, na lingekuwa lengo letu la kudumu kukamilisha utakatifu katika kumcha Mungu. *Mambo ya kidunia, ya kitambo yangekuwa madogo kwa mambo ya mbinguni na ya kudumu.*
*Ninashukuru sana kwa fadhila ya kuwa na uhusianao na kwa namna yoyote ile. Nahisi kupewa heshima kubwa. Ombi langu ni kwamba Bwana kwa rehema Zake kuu na wema wake atanipa nguvu ya kumtumikia.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE WAPENDWA.*
Post a Comment