Amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, JANUARI, 7, 2021
SOMO: KUZITHAMINI AHADI 

Wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu. 

Waefeso 6:6, 7. 



Hebu katika kazi zetu za maisha yote tupambane kwa uthabiti kulijibu ombi la Kristo, kwamba tuweze kuwa na umoja sisi kwa sisi na pamoja naye. Mara zote kabla ya kuanza jambo lolote, tujiulize swali, “Je, hili litampendeza Mwokozi wangu? Je, linapatana na mapenzi ya Mungu?” 



Utambuzi kwamba tunaleta maisha ya Kristo katika uzoefu wa kila siku utaleta hadhi takatifu katika majukumu ya kila siku. Yote tunayofanya yatafanyika kwa uaminifu, ili Bwana aweze kutukuzwa. Kwa namna hiyo tutaonesha kwa ulimwengu kile Ukristo unachoweza kufanya kwa ajili wanadamu wenye dhambi, kuwapatia kwa uthabiti ufanisi unaoongezeka kwa ajili ya utumishi katika maisha haya, kuwaandaa kwa ajili ya maisha ya juu katika ulimwengu ujao.



Ninamsifu Bwana. leo usiku nililala hadi saa kumi kamili. Hakukuwa na kuzinduka kwa kawaida katika usiku. Hii ni baraka kubwa kwangu, ambayo kwayo natoa shukrani. Nimekuwa nikibeba mzigo mzito kadiri ninavyotafakari juu ya hali ya kiroho ya watu wa Mungu, wakishuka chini ya heshima waliyopewa. Nakosa usingizi nikimsihi mwokozi wa mbinguni aje kutusaidia na kuinua wajumbe watakaopeleka ujumbe kwa dhati katika mkazo wake. “Neno lako ndiyo kweli” (Yohana 17:17). Nina shauku kwa ajili ya nguvu na uwezo wa kimwili kwamba toka katika wingi wa moyo uliosukumwa na Roho Mtakatifu kinywa kiweze kunena. 



Mara nyingi katika njozi ya usiku ninazungumza na makundi makubwa na katika wito wenye nguvu ninasisitiza kwa kurudiarudia kwa makundi yaliyo mbele yangu, “Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo yafuateni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtakapofunuliwa pamoja naye katika utukufu. (Wakolosai 3:1—4). 



Ni ahadi bora kiasi gani hii imetolewa kwetu! Basi na tuoneshe kwamba tunazithamini ahadi hizi na kufanya kazi kwa kulenga kikamilifu kwa dhati na kuwa wenye shukrani kwa ajili ya uhakikisho kama huo. Ni kwa manufaa yetu na manufaa ya wote ambao tutakaohusiana nao katika kazi zetu zote za jumuia kwamba tutafunua kuwa tunayatafuta yale mambo yaliyo juu. 

No comments