Fahamu jinsi Amri zilivyoshikwa na Watu mashuhuri katika Biblia

🤔🤔🤔 *HEBU LEO TUJIFUNZE KUHUSU SHERIA KATIKA BIBLIA TAKATIFU NA MATUMIZI YAKE KWA NYAKATI HIZI* 🤔

Hebu tutazame kuhusu amri kumi za MUNGU

*BIBLIA YATAJA WALIOSHIKA AMRI ZA MUNGU NA KUZIFUNDISHA! USIWE KINYUME CHAO!*

1.YESU
"Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, KAMA VILE MIMI NILIVYOZISHIKA AMRI ZA BABA YANGU na kukaa katika pendo lake." 
(Yohana 15:10)

"Mkinipenda mtazishika amri zangu"
(Yohana 14:15)

"...Lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri" (Mathayo 19:17)

"Nao waniabudu bure, wakifundisha Mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu. Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya Wanadamu." (Marko 7:7,8)

2.MTUME PAULO.
"Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (SI KWAMBA SINA SHERIA MBELE ZA MUNGU, BALI MWENYE SHERIA MBELE ZA KRISTO), ili niwapate hao wasio na sheria."
(1 Wakorintho 9: 21)

"Kwa maana naifurahia SHERIA YA MUNGU kwa utu wa ndani." 
(Warumi 7:22)

" Kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa si kitu; Bali kuhifadhi AMRI ZA MUNGU."
(1Wakorintho 7:18)

"Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakao hesabiwa haki." 
(Warumi 2:13)

"Basi TORATI NI TAKATIFU, na ile AMRI NI TAKATIFU na ya haki na njema" ( Warumi 7:12)

3.MTUME PETRO.
"Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, KISHA KUIACHA ILE AMRI TAKATIFU waliyopewa" 
(2 Petro 2:21)

4. MTUME YOHANA.
"Yeye asemaye nimemjua wala HAZISHIKI AMRI ZAKE ni mwongo wala kweli haimo ndani yake."
(1Yohana 2:4)
"Kwa maana Huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba TUZISHIKE AMRI ZAKE, WALA AMRI ZAKE SI NZITO"
(1Yohana 5:3)
"Naye azishikaye AMRI ZAKE hukaa ndani yake yeye, naye ndani yake..."
( 1Yohana 3:24)

MTUME YAKOBO
"Maana mtu awaye yote, atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote ." 
(Yakobo 2:10)

6.ZAKARIA NA ELIZABETI; WAZAZI WA YOHANA MBATIZAJI.
"...Jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa...Elizabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, WAKIENDELEA KATIKA AMRI ZOTE ZA BWANA na maagizo yake bila lawama." 
(Luka 1: 5,6)

7.WATAKATIFU.
"Hapa ndipo penye subira ya WATAKATIFU , HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU , na imani ya Yesu." (Ufunuo 14: 12)

8.IBRAHIMU
"Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na AMRI ZANGU, na hukumu zangu, na sheria zangu." (Mwanzo 26: 5)

9.MUSA, HARUNI NA SAMWELI. 
"Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, na Samweli...
Walipomwita Bwana aliwaitikia;
... alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na AMRI aliyowapa." (Zaburi 99:6,7)

10.AYUBU.
"SIKURUDI NYUMA KUIACHA AMRI YA MIDOMO YAKE . Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu." (Ayubu 23:12)

11.MFALME DAUDI.
"... mtumishi wangu Daudi niliyemchagua,... ALIZISHIKA AMRI ZANGU NA SHERIA ZANGU" (1Wafalme 11:34)

"... mtumishi wangu DAUDI, ALIYEZISHIKA AMRI ZANGU na kunifuata kwa moyo wake wote" 
(1 Wafalme 11:34,38; 14:8)

12.MFALME HEZEKIA.
"Maana alishikamana na BWANA, hakuacha kumfuata, bali alizishika AMRI ZAKE BWANA... 
(2 Wafalme 18: 6)

13.MFALME YOSIA.
"Mfalme... akafanya agano mbele za BWANA, kumtafuta BWANA, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, NA AMRI ZAKE , kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote..." 
(2 Wafalme 23: 3)

"Mfalme...akafanya agano mbele za BWANA, kumfuata BWANA, na kuzishika AMRI ZAKE, na shuhuda zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote..." (2Nyakati 34:31)

14.MFALME ASA
"Basi Asa akafanya yaliyo mema, yaliyo ya adili machoni pa BWANA, Mungu wake. Akawaamuru Yuda wamtafute BWANA, Mungu wa baba zao, na kuzitenda torati na AMRI ."
(2 Nyakati 14: 2,4)

15. MFALME YEHOSHAFATI
"Naye BWANA alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi...alimtafuta Mungu wa baba yake, AKAENDA KATIKA AMRI ZAKE." (2Nyakati 17:3,4)

16.MASALIA WA SIKU ZA MWISHO.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu na kuwa na Ushuhuda wa Yesu..." (Ufunuo 12:17)

17.WAISRAELI WA KIROHO WA KIPINDI CHA AGANO JIPYA.
"Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; NITAWAPA SHERIA ZANGU katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu."
(Waebrania 8:10)

18: MFALME SULEMANI 
"Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe UZISHIKE AMRI ZAKE, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu." (Mhubiri 12:3)

19: NABII ISAYA 
"Na waende kwa SHERIA na Ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi."
(Isaya 8:20)

20:NABII YEREMIA 
"AMRI HIZI ZIKIONDOKA , zisiwe mbele zangu, asema BWANA, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu." (Yeremia 31:36)

No comments