amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, JANUARI, 14, 2021
SOMO: JE, UMEOMBA? 

BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA na kumngojea kwa utulivu.

Maombolezo 3:25, 26.



Bwana anatutaka tuombe ili tupewe. Kuna wajumbe wa kimbingu wanasubiri ombi la dhati ili wasogee karibu na roho yenye njaa na kiu. Kwa hiyo ruhusu moyo wako wote umtafute Bwana. Mngojee Bwana. Wajumbe wa kimbingu watajimimina katika mabomba ya dhahabu yakitiririka katika mabakuli ya dhahabu ili kuwaangazia wengine. Ikiwa utaomba kwa imani utapokea. Kamwe, kamwe usikose mafuta ya dhahabu, kwa kuwa haya yatafanya taa yako iwake. 



Amini mnapokea yale mlioyaomba nayo yatakuwa yenu. Njoo na moyo wa unyenyekevu, lakini kwa kudai ahadi. Kisha amini unapokea. Jina, jina linalopita yote la Mwokozi wetu, ni uhakikisho na ujasiri wetu. Mungu hujielezea kwetu mwenyewe kama msikia maombi. Baki kwenye eneo salama na Mungu, ili uweze kupata ushuhuda wa Roho kwamba wewe ni mwaminifu na miongoni mwa wateule, wale wanaoamini. 



Kamwe usiruhusu Shetani akukatishe tamaa. Usijiweke katika mikono ya M___, lakini katika mikono ya Mungu. Jenga desturi ya kuomba; kuza unyenyekevu na upole; salimisha utunzwaji wa nafsi yako kwa Mungu. Mtegemee Roho Mtakatifu katika yote unayoyafanya, kwa kuwa yeye ndiye nguvu yetu, ufanisi wetu. Bwana mara zote hutufundisha kupitia katika magumu. Omba, omba; kuwa mwepesi katika maombi. Peleka kila kitu kwa Mungu katika maombi—taabu zako za biashara, kukatishwa tamaa kwako, furaha yako, hofu yako. 



Fanya hili, N___ nawe utakuwa na utambuzi wa uwepo wa Mungu, na shukrani zitamiminika toka moyoni na katika midomo yako kwa sauti ya kusifu. Moyo wako utakuwa mchangamfu, nawe utatoa sauti tamu kwa Mungu moyoni mwako. Panda katika viwango vya juu. Usizame katika mazungumzo hafifu, bali ruhusu moyo wako udhihirishe kwa kinywa chako upendo wa Yesu. 



Hebu tuwe wenye busara, wenye kicho, katika kushughulika na Neno la Mungu. Kuna matokeo ya milele katika kutumia ipasavyo talanta zetu za kusema, talanta zetu za sauti, na kila kipawa tulichopewa kutumia na kuendeleza. Tunapaswa kuwa safi katika maneno, watakatifu katika namna zote za mazungumzo, tukimkaribia Mungu naye anatukaribia. 

No comments