amka na Bwana leo 31
KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 31/01/2021
*MUNGU ATAFANYA KAZI PAMOJA NAWE.*
*Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu.* Mwanzo 18:19
🔰 Ningependa kuandika maneno kukuliwaza na kukufariji. Bwana hajakuacha, mikono yake ya milele inakutegemeza. Amekupatia katika maisha ya Ukristo uzoefu ambao ni wa thamani kuu. Umeruhusu nuru yako iangaze katika familia yako, na miali yake ya kiungu kuhisiwa. Bali kuna hatari kwamba utaruhusu upendo wako kwa watoto wako ukusababishe kukubali maombi ambayo utambuzi wako hukwambia kwamba si kwa ajili ya manufaa yao wala kwa utukufu wa Mungu.
🔰 Umekuwa chombo kiteule cha Bwana, ametenda kazi kupitia kwako, na atatenda kwa ajili ya kuokoa roho za watoto wako. Unapaswa kubeba ushuhuda alioubeba Yohana, kurudia maneno ya Kristo kupendana wao kwa wao kama vile Kristo alivyowapenda. Roho Mtakatifu atashuhudia kuhusu umoja wao na Kristo, na waumini na wasio waumini watapata ufahamu toka kwako kwamba umekuwa na Kristo na kujifunza kwake. Kadri unavyofuata na kumjua Bwana, utaakisi tabia ya Kristo.
🔰 Utatawaliwa na udhaifu wa kibinadamu, na bila shaka utafanya makosa, lakini Mwokozi mwenye huruma na upendo atasamehe makosa yako yote, kwa sababu umemwomba, na kwa kuwa unampenda Yesu. Katika roho utapumua upole wa Kristo, nawe utakuwa nuru katika nyumba yako. Mazungumzo yako yatatawaliwa na neema, na upako mtakatifu utatawala maombi yako. Bwana atatenda kazi na juhudi zako kama alivyotenda wakati uliopita, na haki yake itakwenda mbele zako, na utukufu wa Bwana utakuwa tunu yako.
🔘 *Unayo kila sababu ya kumsifu Mungu kwa ajili ya wema na rehema zake. Damu yake inayopatanisha yote ipo kwa ajili ya watoto wako wote. Ikiwa hutatumia nguvu zako za kimwili kupita kiasi, unaweza katika jina la Yesu kufanya kazi kubwa ya thamani... Kwa hiyo kwenu ninyi mnaoamini, Yeye ni wa thamani... Tembeeni katika upendo kama watoto wapendwa. Roho wa Mungu anapambana na watoto, akiwaalika kwa Kristo, akisema, “Njooni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari” (Luka 14:17). Je, hautatii?*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment