ALBERT CHALAMILA AUNDA TUME NDOGO

MKUU WA MKOA MBEYA AUNDA TUME KUFWATIA KIFO CHA DEREVA.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameunda tume ndogo ya watu wanne na kuipa jukumu la kuchunguza kifo cha dereva wa Lori aliyefahamika kwa jina la Abdulhman Issa anayedaiwa kufia mikononi mwa polisi katika eneo la Shamwengo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Chalamila amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha askari polisi wakimshusha kwenye gari dereva huyo na hatimaye kubainika amefariki na mwili wake kuhifadhiwa katika hospitali ya Igawilo jijini Mbeya.

Akizungumza na wanahabari hii leo Chalamila amesema Tume aliyoiunda itampa majibu ndani ya siku tatu kuanzia leo na endapo itabinika kuwa dereva huyo amefia kwenye mikono ya vyombo vya dola wahusika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
#BinagoUPDATES

No comments