amka na Bwana leo 28

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi 28/01/2021

*BWANA, WEWE UNALIJUA HILI FIKA*

*Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.* Waefeso 6:12

📜 Tangu nilipofika kwenye mkutano huu [mkutano wa kila baada ya miaka miwili, Unioni Konferensi ya Pacific], nimepitia uzoefu wa ajabu. Siku moja, baada ya kutokea mbele ya mkutano ili kusoma jambo fulani kwenu, mzigo uliokuwa moyoni mwangu uliendelea kunielemea baada ya kurudi katika chumba changu. Nilikuwa katika mfadhaiko wa moyo. Siku hiyo si nilipoteza usingizi wangu kabisa. 

📜 Ilionekana kana kwamba malaika waovu walikuwa ndani kabisa ya chumba nilichokuwa. Na nilipokuwa nikiteseka moyoni, ilionekana kana kwamba ninapitia maumivu makali sana ya kimwili. Mkono wangu wa kulia, ambao kwa miaka mingi umetunzwa dhidi ya magonjwa na maumivu, ulionekana kukosa nguvu. Nisingeweza kuuinua. Kisha nikapata maumivu makali sana katika sikio; kisha maumivu ya kutisha katika taya. Ni kama nilipaswa kupiga kelele. Bali niliendelea kusema, “Bwana, wewe unalijua hili fika.” 

📜 Nilikuwa katika mateso makali. Ilikuwa kana kwamba ubongo wangu na kila sehemu ya mwili wangu ilikuwa na maumivu. Wakati mwingine niliweza kuinuka, na kufikiri, “Sitalala hapa wakati mwingine.” Kisha nikafikiri, “Utaamsha tu wale ambao wako ndani ya nyumba, na hawezi kukufanyia chochote.” Na hivyo nikaendelea kumtazama Bwana, na kusema, “Bwana, wewe wajua kuhusu maumivu haya.” Maumivu yaliendelea, wakati huu katika taya, kisha katika ubongo, kisha katika sehemu zingine za mwili, mpaka karibia kupambazuka. Kabla hakujapambazuka nilipata usingizi kama kwa saa moja. 

📜 Mkono wangu uko salama asubuhi hii. Majeshi yaa malaika waovu yalikuwa katika kile chumba, na kama nisingemtazama Bwana kwa imani, sijui nini kingenipata... 
Sitaweza kuwapa maelezo kuhusu majeshi ya Shetani yaliyokuwa kazini katika kile chumba,.. lakini tangu niliposimama mbele yenu asubuhi ilivofuata, sijawa na maumivu. 

🔘 *Nuru imekuwa ikinijia kwamba tusipokuwa na udhihirisho mkubwa wa utendaji wa Roho wa Mungu, na udhihirisho mkubwa wa nguvu ya kiungu ukitenda kazi miongoni mwetu, wengi wa watu wa Mungu watashindwa. Mawakala wa kishetani wataingia ndani, kama walivyokuja kwangu. Lakini hatuwezi kudiriki kujisalimisha kwa nguvu ya adui.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments