RUSHWA YA NGONO KUWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI
Imeelezwa kuwa watakaokamatwa kwa makosa ya rushwa ya ngono kuanzia sasa watafunguliwa shtaka la uhujumu uchumi.
Hayo yameelezwa na mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoa wa Kilimanjaro, Furahini Kibonga katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Alisema kosa la kuomba rushwa ya ngono sasa litafunguliwa shitaka kama kosa la uhujumu uchumi kutokana na matokeo ya rushwa hiyo katika utekelezaji wa majukumu na uzalishaji.
“Rushwa ya ngono inasababisha kupata wasomi ambao hawana sifa, pili kuajiriwa watu ambao hawana sifa na wenye sifa wanaachwa, na pia wale wanaoajiriwa uzalishaji wao na utendaji kazi ni mdogo na hivyo kusababisha uzalishaji mdogo na uchumi wa taifa kuwa mdogo,” alisema Kibonga.
#BinagoUPDATES
Post a Comment