amka na Bwana leo 26

KESHA LA ASUBUHI

JUMANNE, JANUARI, 26, 2021
SOMO: PASIPOTI YA KWENDA MBINGUNI

Kwa maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kwa wingi sana, tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu, bali visivyoonekana ni vya milele. 

2 Wakorintho 4:17, 18.



Ninazungumza nanyi na watoto wenu. Ninawahurumia katika msiba wenu wa wakati huu, kama ningekuwa pamoja nanyi, ningesema maneno ya faraja kwenu, lakini kwa vile sipo nanyi, ninaweza tu kuandika mistari michache, na kuwajulisha kuwa siwasahau katika mateso yenu.... 



Tuko katika jioni ya historia ya dunia hii, na tunaweza kuwazika wafu wetu, tukijua kuwa wamefichwa kwa muda kitambo tu hadi uchungu upite. Hatupaswi kuwaombolezea kama wale wasio na tumaini; kwa kuwa maisha yao yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Tuna kila sababu ya kushangilia.... 



Magumu ambayo wale walio ndani ya Kristo na kuzishika amri zake wanapaswa kuyapitia, hayatengenezwi na Kristo. “Mtu ye yote akitaka kunifuata,” Anasema, “na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate” (Mathayo 16:24). Wajibu wa nafsi yenye uadilifu ni kushikilia kweli, kutenda kwa adili. Tunazaliwa na ukosefu wa ari ya kutenda vyote viwili. Inahuzunisha kugundua katika utendaji wa mtu mwenyewe upinzani wa sifa za kimaadili zinazokubalika mbele za Mungu, kama utii, upendo, utu wema, na uvumilivu ambao hauwezi kukasirishwa. Jiambieni wenyewe, na watoto wenu, mimi ni mdhaifu, bali Mungu ni nguvu yangu. Amenipatia sehemu yangu ya wajibu. Kamanda mkuu ninayemtumikia anahitaji niwe mshindaji.... 



Ruhusu mateso yaliyofika katika jamaa ya familia yako yawe baraka kwenu wote. Dada yetu mpendwa, mama yako, alimpenda Yesu. Vita yake imekoma. Unapaswa kukumbuka kwamba amelala katika tumaini. “Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu” (Wakolosai 3:4). Ruhusu amani na faraja ya Roho Mtakatifu zije mioyoni mwenu. Fungua milango ya mioyo yenu, ili Yesu aingie kama mgeni wa heshima, nanyi mtakuwa na mfariji. “Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi” (Yohana 15:12). Hebu mioyo ya wenye uhai ikaribiane kwa kila mmoja. Kila mmoja na ajaribu kuwa baraka kwa mwingine, na si kikwazo.... 



Hebu tujiandae kwa ujio wa Mwana wa Adamu. Hebu tuwe thabiti kwa Mungu, nasi tutapata taji ya uzima. 

No comments