amka na Bwana leo 24
KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 24/01/2021
*WAKAMILIFU KATIKA YEYE*
*Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.* Mathayo 5:48
🔰 Mungu anahitaji ukamilifu wa kimaadili kwa wote. Wale waliopewa nuru na fursa wanapaswa, kama mawakili wa Mungu, walenge kuwa wakamilifu, na kamwe, kamwe wasishushe kiwango cha haki ili kutoa nafasi kwa mielekeo ya makosa ya kurithiwa na mazoea. Kristo alichukua juu yake asili yetu ya ubinadamu, na kuishi maisha yetu, kutuonesha kuwa tunaweza kuwa kama yeye kwa kushiriki katika asili ya uungu. Tunaweza kuwa watakatifu, kama Kristo alivyokuwa mtakatifu katika asili ya mwanadamu. Kwa nini basi kuna tabia nyingi zinazotofautiana duniani? Ni kwa sababu hawahisi kwamba njia zao zinazotofautiana na mbaya, usemi usio wa upole ni matokeo ya moyo usio mtakatifu...
🔰 Ni harufu nzuri ya upendo wetu kwa wanadamu wenzetu ndiyo hufunua upendo wetu kwa Mungu. Ni uvumilivu katika kazi ndio huleta pumziko katika roho. Ni kupitia kwa wapambanaji wanyenyekevu, wenye bidii, waaminifu ustawi wa Israeli hujengwa. Mungu hushikilia na hutia nguvu yeyote anayewiwa kujifunza njia ya Kristo...
🔰 Uvumbuzi wote wa kweli na kupiga hatua vina chanzo chake katika yeye aliye wa ajabu katika mashauri na bora sana katika utendaji. Lolote tunalofanya katika idara yoyote ya kazi tuliyowekwa Mungu hutamani kututakasa na kutupandisha hadhi. Anatamani kutawala akili ya mwanadamu, ili kwamba aweze kutenda kazi kamilifu.
🔰 Mguso laini wa mkono wa tabibu, uweza wake juu ya neva na misuli, ufahamu wake wa viungo dhaifu vya mwili, ni hekima ya uweza wa kiungu, ni kwa ajili ya kutumiwa kwa niaba ya wanadamu wanaoteseka. Ujuzi wa seremala kutumia nyundo, nguvu ambayo mfua vyuma hutumia kutengeneza fuawe, hutoka kwa Mungu. Amewapatia wanadamu uwezo, na anatarajia kwamba watafute mashauri kwake. Hivyo wataweza kutumia vipawa vyake kwa namna sahihi, kushuhudia kwa utukufu wa Mungu kwamba wao ni watenda kazi pamoja naye. Hivyo husafisha mioyo yao kwa utakaso wa Roho kupitia katika kweli. Katika uzoefu wao, maneno ya Kristo yanatimilizwa, Wenye moyo safi watamwona Mungu. (Tazama Mathayo 5:8)
🔘 *Wote wanapaswa kujisikia kwamba wanatenda kazi kwa ajili ya kusudi moja kuu. Kazi katika kila idara ni ya Mungu, na wote wanaofanya kazi hiyo kwa ukamilifu, bila makosa, huwakilisha ukamilifu wa Mungu.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️
Post a Comment