MWANAFUNZI PAUL LUZIGA APOKELEWA KIFALME MKOANI MBEYA
Paul Cosmas Luziga Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne amepata mapokezi ya kifalme alipowasili shule aliyekuwa akisoma Panda Hill katika Bonde la Songwe mkoani Mbeya.
Mwanafunzi huyo ambaye wakati matokeo yalipotoka alikuwa jijini Dar es Salaam, amelazimika kurejea mkoani Mbeya kwa ndege baada ya uongozi wa shule yake kumlipia tiketi ya usafiri ya kwenda na kurudi ili wampongeze.
Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), mwanafunzi huyo alishuhudia maajabu baada ya kukuta magari zaidi ya 20 aina ya Coaster yakiwa yamewabeba wanafunzi wenzake zaidi ya 500 na walimu wao waliofika uwanjani kumpokea.
#BinagoUPDATES
Post a Comment