mafunzo ya watu wazima leo 24
LESONI, JANUARI 24
SOMO: MWISHO WA HUZUNI KWA AJILI YA GALILAYA (ISA. 9:1—5)
Kwa nini Isaya 9:1 inaanza kwa neno (lakini) linaloashiria kinyume cha kile kinachoitangulia?
Isaya 8:21, 22 huelezea hali isiyokuwa na tumaini ya wale wanaogeukia ibada ya mashetani badala ya Mungu wa kweli: popote watakapotazama, wataona “shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa” (Isa. 8:22). Kinyume chake, kutakuja wakati ambapo “yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko” (Isa. 9:1). Watu wa ukanda wa Galilaya wamebainishwa hapa kama watu wanaopokea mbaraka wa kipekee wa “nuru kuu” (Isa. 9:2). Taifa litazidishwa na kufurahia kwa sababu Mungu atakuwa ameivunja “fimbo yake yeye aliyemwonea” (Isa. 9:4).
Ukanda wa Galilaya unaoneshwa hapa kwa sababu ulikuwa miongoni mwa maeneo ya kwanza ya Israeli kutekwa. Kama jibu kwa ombi la Ahazi kwa ajili ya msaada, Tiglath-pileseri III aliiteka Galilaya na maeneo yaliyoko pande zote za Jordani kaskazini mwa Israeli, alichukua baadhi ya mateka, na aliyageuza maeneo hayo kuwa majimbo ya Ashuru (2 Wafalme 15:29). Hivyo, ujumbe wa Isaya ni kuwa eneo lililokuwa la kwanza kutekwa litakuwa la kwanza kukombolewa.
Mungu anamtumia nani kuwakomboa watu Wake? Isa. 9:6, 7. Ni lini na kwa namna gani unabii wa Isaya 9:1—5 ulitimizwa? Mat. 4:12—25.
Siyo kwa bahati mbaya, huduma ya awali ya Yesu ilikuwa katika ukanda wa Galilaya, mahali ambapo alitoa tumaini kwa kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu na kwa kuponya watu, ikiwa ni pamoja na kuwakomboa wenye pepo kutoka utumwa wa ibada ya mapepo (Mathayo 4:24).
Hapa ndipo tunaona mfano mkamilifu wa jinsi Biblia inavyochukua matukio yaliyotokea katika nyakati za Agano la Kale na kuyatumia kama mifano ya matukio yaliyotokea katika nyakati za Agano Jipya. Bwana aliunganisha mifano ya zama moja na ya zama nyingine, kama vile katika Mathayo 24, wakati Yesu alipounganisha uangamizaji wa Yerusalemu mwaka B.K. 70 na uangamizaji wa wakati wa mwisho wa ulimwengu.
Ikiwa mtu angekuuliza, Yesu amekukomboa kutoka katika jambo gani, ungemjibuje? Ni ushuhuda gani binafsi unaweza kuutoa kuhusu nguvu ya Kristo katika maisha yako?
Post a Comment