binti mchawi
KISA CHA BINTI MCHAWI, INATISHA
Dada mmoja mfanyakazi wa serikali alikuwa na mtoto mdogo hivyo ikambidi atafute housegirl, aliagiza housegirl kutoka kijijini kwao, binti wa kazi alikuwa mchapakazi ila yule dada mama mwenye nyumba alianza kupata hofu kila siku alihisi mle ndani ya nyumba yake toka amlete housegirl kulikua na dalili ya nguvu za giza.
Familia ilianza kupata misukosuko ya ajabu ajabu mume wake alianza kulalamika maumivu makali ya mgongo mtoto wake nae akaanza kukonda mfululizo,
Hakumtilia shaka moja kwa moja binti yule ila alijitahidi kuongeza maombi na sala kila alipoenda ibadani.
Siku moja kanisani akiwa anaombewa mchungaji alimwambia chanzo cha kuugua mtoto wako naoneshwa kwenye maono kuwa umemkaribisha shetani ndani kwako. Dada yule alistaajabu ndipo akamueleza mchungaji kuwa siku za karibuni aliletewa housegirl toka kijijini ila hakuwahi kumtilia shaka mchungaji akamwambia HUYO NDIO AGENT WA SHETANI NDANI YA NYUMBA YAKO.
Basi kesho yake dada yule alimuaga housegirl wake kama kawaida akaenda kazini ila siku hiyo alimshtukiza na kurudi ghafla mida ya saa 5 asubuhi akiongozana na mchungaji wake pastor Emanuel Msoka ambaye ndiye Admin wa Online News Tz page inayoongoza kwa simulizi kali za kusisimua Tanzania, walichungulia dirishani sebuleni wakamuona mtoto kafungwa kamba kwenye kiti alafu housegirl yupo mezani anakula huku akiongea na mtu asiyeonekana. Walistaajabu. mchungaji akanyata hadi mlangon akasukuma mlango kuingia bahati nzuri ulikua haujafungwa
Housegirl alistuka akakurupuka na kutaka kukimbilia chumbani kwake akiwa kashika kopo lenye rangi ya udongo, mchungaji akampiga mtama na kumnyang'anya kopo lile , mchungaji alipolifungua akatoka nyoka mweusi kutoka kwenye lile kopo, mchungaji akaanza kumshambulia yule nyoka huku akimkemea kwa jina la YESU. Nyoka alipozidiwa na kukaribia kufa housegirl alilia sana akamwambia mchungaji, "Naomba msimuue huyo nyoka, sio nyoka ni mdogo wangu"
Walistaajabu wakamtandika wakamwambia aseme, housegirl akasema yule nyoka ni mdogo wake alipewa na bibi yake aje nae mjini maana kijijini maisha magumu, kwa hiyo alikuwa akimuhifadhi kwenye kopo kama nyoka ila mabosi wakiondoka anambadilisha kuwa mtu wanapika na kula pamoja ila mtoto wa boss alikuwa akimfunga kwasababu alikuwa anaogopa sana na kulia kila akimuona yule nyoka, maskini kumbe kitoto cha boss kilikuaga kinashuhudia makubwa tatizo hakijui kuongea bado. Alikiri pia huwa usiku anaingiaga chumbani kwa boss kimiujiza anamshusha mke wa boss uvunguni mwa kitanda kisha anachukua sura yake na kumpumbaza mume (boss) na kumhadaa wanafanya mapenzi usiku kucha mume akijua anafanya na mkewe kumbe ni housegirl ndio maana boss ameanza tatizo la kuugua mgongo.
Baada ya maelezo ya binti, walimwambia amgeuze nyoka kuwa mtu wamuone ndipo akamtakia maneno ya kimila, "dhoruaaamira moorianguvaaarihoikaaatuzaaaruemo, Husna" ghafla akabadilika akawa binti mdogo mwenye makovu ya kipigo cha pastor jina anaitwa Husna. Walipoulizwa malengo yao ya baadaye yalikua yapi wakasema mwisho wa mwaka walikua wanatarajia kumla nyama mtoto wa boss yaan angeugua ghafla afe. Majirani na jamii ililIstaajabu, hakika mahousegirl tunaowaajiri inabidi kuwachunguza watokapo wengine ni maagent wa shetani.
Ndugu msomaji ninakuombea Mwenyezi Mungu akufunulie maagent wa shetani waliotumwa katika maisha yako au mipango yako ili kukuangamiza akawaumbue na kuwaaibisha kila utakapomuomba Mungu akakufanikishe kuwatambua na kuwashinda, tafadhali kama ungependa ulinzi wa Mungu juu yako kuanzia leo sema AMEN kisha SHARE ujumbe huu uwafikie watu wote kwenye jamii
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
IMEANDIKWA NA MWALIMU HABELNOAH
FROM ROCK CITY MWANZA
JM LIBRARY
Post a Comment