WALIOPANDISHA BEI YA SARUJI KUSAKWA
WALIOPANDISHA BEI YA SARUJI KUSAKWA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amewajia juu wafanyabiashara wa saruji waliopandisha bei na kuagiza wakuu wa wilaya kuendesha msako kwenye maeneo yao.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Kuzalisha saruji cha Kilimanjaro na kupata taarifa kwamba kiwandani hapo bei haijapanda hivyo wafanyabiashara wameamua wenyewe kupandisha bei.
Miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa kwa watakaobainika kupandisha saruji hiyo ni pamoja na kufungiwa leseni za biashara.
Post a Comment