amka na Bwana

#KESHA_LA_ASUBUHI

Alhamisi 03/09/2020

*KUTAKASWA KUPITIA UTII*

*Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.*
Mambo ya Nyakati 20 : 7, 8

🔰 Adamu na Hawa walithubutu kukiuka matakwa ya Bwana, na matokeo ya kuogofya ya dhambi yao yapaswa kuwa onyo kwetu tusifuate mfano wao wa kutokutii. Hakuna utakaso wa dhati isipokuwa kupitia utii kwa ile kweli. Wale wanaompenda Mungu kwa moyo wote watazipenda sheria zake zote pia. Moyo uliotakaswa huwa na mapatano na sheria ya Mungu; kwa kuwa ni takatifu, adilifu na njema. 

🔰 Hakuna hata mmoja ambaye ana kicho na upendo wa kweli kwa Mungu atakayeendelea kuasi sheria kwa namna yoyote ile. Pale ambapo mwanadamu anaasi anakuwa chini ya hukumu ya sheria, na inakuwa kwake nira ya utumwa. Haidhuru awe mtu wa fani gani hawezi kuhesabiwa haki, yaani kupata msamaha. 

🔰 "Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi." Kwa kupitia utii huja utakaso wa mwili, nafsi na roho. Utakaso huu ni kazi inayoendelea, na ukuaji kutoka hatua moja ya ukamilifu kuelekea hatua nyingine. 

🔰 Hebu imani hai kama nyuzinyuzi za dhahabu ionekane hata katika utendaji wa majukumu madogo madogo. Ndipo kazi zote za siku kwa siku zitasaidia ukuaji wa Kikristo. Kutakuwa na kudumu katika kumtazama Yesu. Upendo kwake utatoa nguvu kwa kila jambo litakalotendeka. Ndipo kwa matumizi sahihi ya vipawa vyetu twaweza kujifungamanisha na ulimwengu wa juu kwa mnyororo wa dhahabu. Huu ndio utakaso halisi, kwa kuwa utakaso ni kutenda kwa furaha majukumu ya kila siku katika utii mkamilifu wa mapenzi ya Mungu. 

🔘 *Wakati inapokuwa kusudio la moyo kumtii Mungu, wakati ambapo juhudi zinaelekezwa katika kulitekeleza, Yesu anakubali nia na juhudi hizi kama huduma bora kabisa, naye huondoa mapungufu kwa tabia yake njema ya kimbingu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments