amka na Bwana
#KESHA_LA_ASUBUHI
Jumatano 02/09/2020
*MFANO WA KIVITENDO WA UTAKASO*
*Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.* Waefeso 5:22 - 27
☄️ Hapa upo utakaso wa kibiblia. Sio jambo la kujionesha tu au kazi ya nje. Ni utakaso unaopokelewa kupitia njia ya kweli. Ni ukweli unaopokelewa ndani ya moyo na kutekelezwa kwa vitendo katika maisha.
☄️ Yesu, akichukuliwa kuwa mwanadamu, alikuwa mkamilifu, lakini alikua katika neema. Luka 2:52: "Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu." Hata Mkristo aliye bora kabisa aweza kudumu kukua katika kumwelewa na kumpenda Mungu.
☄️ "Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una Yeye sasa na hata milele." Utakaso sio kazi ya kufumba na kufumbua, au saa moja au siku moja. Ni ukuaji usio na kikomo katika neema. Hatuwezi kujua vile pambano linalofuata litakavyokuwa.
☄️ Shetani yuko hai, na anatenda kazi, na kila siku tunapaswa kufanya jitihada ya kumlilia Mungu kuomba msaada na nguvu za kumpinga. Ilimradi shetani angali anatawala sharti tudhibiti ubinafsi, vizuizi vya kushinda na hakuna sehemu ya kupumzika, hakuna sehemu ambayo twaweza kuifikia na kusema tumekwisha kufanikiwa. Maisha ya Mkristo ni mwendo wa daima. Yesu anadumu kama Msafishaji na Mtakasaji wa watu wake. Na sura yake inapodhihirishwa kikamilifu kwao, wamekuwa wakamilifu na watakatifu, walioandaliwa kwa ajili ya kupaa mbinguni.
🔘 *Kila Mkristo hai ataendelea kukua katika maisha matakatifu. Kadiri anavyokua kuelekea ukamilifu, anapitia uzoefu wa uongofu kwa Mungu kila siku; na mabadiliko haya hayakamiliki hata atakapofikia ukamilifu wa tabia ya Kikristo, maandalio kamili kwa ajili ya hatua za mwisho za kufikia kutokufa.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment