je unajua kama hizi ni siku za mwisho,au umepofuka?

#WAADVENTISTA #WASABATO #TUNAONA NINI????

PIA ENYI WATU MSIO NA DINI #MNAONA NINI??

BWANA awabariki sana wasomaji wangu. MUNGU awapiganie na awashindie kila jaribu la Shetani . Ninyi ni wana na binti za MUNGU , mnaye BABA mwenye nguvu💪🏻 Juu mbinguni. Shetani hana lolote. Basi karibuni tena katika somo tajwa hapo juu.👆🏻👆🏻

Waamuzi 9:36-37
👉🏻 Basi Gaali alipowaona hao watu akamwambia Zebuli, Tazama watu washuka toka katika vilele vya milima, Zebuli akamwambia, ni kivuli cha milima unachokiona kama ndio watu. Kisha Gaali akasema mara ya pili, akanena, watu washuka katikati ya nchi, na kikosi kimoja kinakuja kwa njia ya mwaloni wa meonenimu.

👉🏻Huu ni mfano mzuri wa makundi mawili tunaoishi zama hizi za mwisho. Kundi la Gaali linaona hatari inayoijia dunia kwa haraka, lakini kundi la Zebuli linaona amani na vivuli.

Kauli ya zebuli ndiyo kauli ya WACHUNGAJI na washiriki waliolala kiroho na watu wa ulimwengu pia.

MUNGU ametuma wajumbe kama akina Gaali kutangaza hali ya hatari iliyo mbele yetu, lakini kundi la akina zebuli ndani ya kanisa na nje ya kanisa linasikika likisema hakuna kitu kama hicho, linasema hakuna hatari yoyote, bali ni amani na salama na vivuli tu, kivuli cha milima ndicho hili kundi la zebuli linachoona.

Ndugu msomaji, unaona nini duniani???

Je unaona adui akituzingira?? Au unaona kivuli cha milima!

Hatari inaijia dunia yetu, hatari inawajia wakazi wa dunia hii, hatari inawajia washiriki wa kanisa la MUNGU , lakini wengi wao hawaoni hatari, bali wanaona vivuli vya milima.

Lakini pia milima katika unabii inawakilisha makanisa. Isaya 2:2-3.

Maana rahisi ni kwamba, watu wengi wanaona harakati zinazofanywa na umoja wa mataifa, Viongozi wa dini, na wanasiasa wao, lakini hawaoni lolote ndani ya harakati hizo, bali wanaona vivuli vya makanisa, hawaoni adui aliye ndani ya hayo makanisa yanayoshirikiana na wanasiasa wa dunia hii, wao wanaona ni vivuli tu, wanadhani ni harakati za kidini na amani , hawaoni Adui aliyejificha nyuma ya makanisa yao na nyuma ya wanasiasa, adui ambaye anatunyemelea kama simba aungurumaye. Ee ndugu unaona nini???

Washiriki pamoja na wasiomcha MUNGU , wote wamelala usingizi wa amani na salama.

Zekaria 1:9-11👉🏻 Ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, ni nani hawa??? Basi yule MALAIKA aliyesimama pamoja nami akaniambia, nitakuonyesha ni nini hawa. Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, hawa ndio BWANA aliowatuma, waende huko na huko duniani . Nao wakamjibu yule MALAIKA wa BWANA aliyesimama kati ya mihadasi, wakasema, Tumekwenda huko na huko duniani, na tazama, dunia yote inatulia, nayo imestarehe.

👆🏻👆🏻Huu ni ukweli usiopingika ya kwamba wanadamu wengi hawajui wakati tulio nao, hawajui hatari inayotujia, hawajui mwisho unakuja haraka ajabu mno. Wajumbe wa mbinguni huzunguka huko na huko duniani kuona kama kuna watu waliojiandaa kuihama hii Dunia , lakini wanaona watu wote wametulia na kustarehe bila habari yoyote ya kuwa mwisho unawaijia haraka na kwa ghafla.

Tunao mda mchache wa kufanya kazi ya MUNGU na kujisahihisha katika matendo yetu, mawazo yetu. BWANA anakuja upesi.

Wengine wa washiriki wanatazamia kuja kwa YESU kuko mbali mno, hivyo mioyo yao imetupilia mbali ukweli wa leo na hivyo wamejiungamanisha na ulimwengu huu na wanatenda kama wa ulimwengu huu.
                  Maandiko ya Awali. Uk 54-55.

👉🏻 Gaali aliwaona maadui wakiwazingira, Zebuli akaona ni vivuli na salama tu, je ndugu msomaji, wewe unaona nini?? Unaona amani au unaona adui akitunyemelea!

👉🏻 Muda siyo mrefu tutaingia katika jaribio kuu la Imani yetu. Kila mwanadamu aliye hai atahusika.

Kundi la Gaali wao kila siku wapo macho na wanajiandaa kwa Bwana, kukesha na kujifunza neno la MUNGU .

Kundi la zebuli wao hawana maandalizi, wanaona vivuli vya amani na salama duniani huku wakizidi kujiungamanisha na ulimwengu kila siku.

Kundi la Zebuli hawataweza kusimama katika siku ya jaribio kuu lililo mbele yetu maana hawakujiandaa.

1wathesalonike 5:1-6
👉🏻 Wakati wasemapo amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo ghafla..

Leo dunia nzima inahubiri amani, wanasiasa wanahubiri amani, makanisani wanahubiri amani, MUNGU yeye anasema, wakati wasemapo amani na salama, ndipo uharibifu unapokuja juu yao.

👉🏻 Neno la MUNGU linasema hakutakuwa na amani wala salama katika dunia hii. Neno la MUNGU huwa halikosei. Mikakati kabambe inafanywa kimya kimya ili kuwaleta Wanadamu wote katika ibada ya Jumapili. 

Uwe macho kama Gaali.
YESU yuaja
Na ujira wake u pamoja naye.

BWANA awabariki 😅🙏🏻

No comments