amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Ijumaa 04/09/2020
*MATUNDA YA UTAKASO*
*Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, furahini.* Wafilipi 4:4
📚 Kupitia kwa Yesu wana wa Adamu walioanguka wanafanywa kuwa "wana wa Mungu." "Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake. "Maisha ya Kikristo yapasa yawe ya imani, ushindi na furaha katika Mungu. "Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu."
📚 Ni kweli aliyosema mtumishi wa Mungu Nehemia, "kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu." Na Paulo anasema "Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, furahini," "furahini siku zote. Ombeni bila kukoma. Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." Hayo ndiyo matunda ya uongofu na utakaso wa kibiblia. Asili ya binadamu (mwenye haki kweli kweli) hujazwa upendo kwa Mungu na wanadamu wengine naye hutenda kazi za Kristo kwa hiari.
📚 Wale wote ambao huja karibu na mvuto wake hutambua uzuri na harufu njema ya maisha yake ya Kikristo, wakati ambapo yeye mwenyewe hana utambuzi wa jambo hilo, kwa kuwa linapatana na tabia yake na yale anayoyapenda. Huomba nuru kutoka mbinguni, naye hupenda kutembea katika nuru hiyo. Ni chakula na kinywaji chake kuyafanya mapenzi ya Baba yake aliye mbinguni. Maisha yake yamefichwa na Kristo katika Mungu; hata hivyo hajivuni kwa hili, wala kuonekana kujua hilo.
🔘 *Mungu anafurahishwa na wale ambao ni wapole na wanyenyekevu ambao wanafuata kwa ukaribu nyayo za Kiongozi wao. Malaika wanavutiwa nao na wanapenda kudumu katika njia zao. Wanaweza kupitwa kama wasio na thamani ya kutambuliwa na wale wanaodai kufikia viwango vya juu ambao wanafurahia kutangaza umaarufu wao; lakini malaika wa mbinguni huwainamia kwa upendo na huwa kama boma la moto kuwazunguka....Mwanadamu amepewa fadhila ya kuwa mrithi kwa Mungu na mshiriki wa urithi pamoja na Kristo.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment